January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yawaita walioibiwa kura

Spread the love

WANASIASA ambao walikuwa wakigombea nafasi za ubunge na udiwani, wenye mashaka na kushindwa kwao wanatakiwa kuwasilisha mashauri yao katika mahakama husika ndani ya siku tatu baada ya kutangazwa kwa matokeo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Fredinand Wambali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Majaji, mahakimu na wasajili wa mahakama pamoja na mawakili wa serikali.

Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na UNDP, Wambali amesema watumishi hao wanapatiwa mafuzo kwa lengo la kuwaongezea ueledi wa kukabiliana na kesi za uchaguzi ili kuhakikisha hazichukui muda mrefu.

“Tupo hapa mjini Dodoma kwa ujumla yetu ambao ni majaji, mahakimu, wasajiri na mawakili wa serikali ili kuweza kupata ueledi na kujua utaratibu uwa utatuzi wa migogoro ya uchaguzi kitaifa na kimataifa,” amesema Jaji Wambali.

Amesema kupitia shirika lisilokuwa la kiserikali UNDP kuwawezesha kupata mafunzo hayo ili kuhakikisha wanasheria hao wanafanya kazi yao kwa ueledi mkubwa wa kushughulikia migogoro hiyo ya kisiasa.

Jaji Wambali amesema ili mlalamikaji aweze kusikilizwa shauri lake anatakiwa kuwasilisha malalamiko yake ndani ya siku 30 tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Jambo lingine amesema ili kufungua kesi la malalamiko ya uchaguzi kwa ngazi ya ubunge unatakiwa kulipa ada ya Sh. 200,000 huku diwani akitakiwa kulipa Sh. 100,000.

Amesema mbali na kulipa ada lakini pia inatakiwa yule anayeshitaki aweke kinga ya uchaguzi Sh. 5 milioni kwa yule ambaye amemshitaki.

Kwa upande wake mwakilishi wa UNDP, Awa Dabo amesema waendesha mashitaka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kesi za uchaguzi wanatakiwa kutenda haki bila kuwa na upande wowote.

Amesema wale wote ambao wanapokea kesi za uchaguzi lazima wazitendee haki kwa ajili ya kutenda haki kwa kupitia vyema nyaraka mbalimbali ambazo zitatoa mwelekeo ya kesi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Devisioni ya Madai, Obadia Kimeya amesema kwa sasa wameshapokea kesi za uchaguzi 5.

Amesema wanaendelea kupokea kesi hizo na kutokana na mafunzo ambayo wawanayapata majaji, mahakimu na mawakili wa serikali haki itatendeka na sheria zitafutwa zaidi.

error: Content is protected !!