Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yatupilia mbali ombi la kina Mbowe kumkataa shahidi
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yatupilia mbali ombi la kina Mbowe kumkataa shahidi

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi, katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, dhidi ya shahidi wa sita wa jamhuri. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pingamizi hilo limetupwa leo Alhamisi, tarehe 4 Novemba 2021 na mahakama hiyo mbele ya Jaji Joackim Tiganga.

Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo, Jaji Tiganga amesema ni msimamo wa sheria kuwa pale ambapo ushahidi unakuwa haujasomwa basi hauwezi kupokelewa mahakamani labda kama wataomba kama ilivyoelezwa na Wakili Mtobesya Kwenye Kifungu cha 289 CPA.

Amesema, jambo linalobishaniwa ni kwamba ushahidi haukusomwa hapa Mahakamani. Mahakama inayo jukumu la kukagua kama ushahidi ulisomwa au haukusomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakati wa commital inasoma.

Amesema, Mahakama wakati ina- examine records imeona kwenye ukurasa wa 21 kwamba maneno yafuatayo kwamba ushahidi na mashahidi yamesomwa kwa washitakiwa. Akasema Hakimu Simba tarehe 23 mwezi wa nane mwaka 2021.

Jaji Tiganga ameendelea kusema kuwa, akaorodhesha mashahidi 21 na jina la shahidi namba sita linaonekana katika ukurasa wa 31. Na kwamba mashahidi hao waliorodheshwa na maelezo yao yalisomwa mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

         Soma zaidi:-

Huo ndio msimamo na kumbukumbu za Mahakama, kwamba maelezo yote yalisomwa na kwamba ushahidi huo ulisomwa na Mahakama haikuishia hapo, kama nilivyosema katika ku- examine.

Mahakama ikaona kuna maelezo ya shahidi namba sita. Kumbe yalisomwa na kwamba tatizo maelezo hayo hayakuunganishwa katika kifurushi cha commital proceedings.

Jaji Tiganga akihitimisha hoja hiyo amesema, kutokwemo katika kifurushi haimaanishi kwamba ushahidi wa shahidi namba sita haukusomwa.

“Hivyo Mahakama inaona pingamizi halina mashiko. Lengo la pingamizi ilikuwa ku- impeach record za Mahakama. Maelezo yaliyopo mahakamani yanaonesha kwamba ushahidi ulisomwa, hivyo naelekeza sasa shahidi aendelee,” amesema Jaji Tiganga

Mbali na Mbowe, katika kesi hiyo wengine ni, Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya ambao walikuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pingamizi hilo liliibuliwa na wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya, wakati shahidi wa sita wa Jamhuri, SSP Sebastian Madembwe, akitoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Alipokuwa akitoa ushahidi wake, Wakili Mtobesya aliibua hoja ya pingamizi dhidi ya shahidi huyo, akidai kwamba ushahidi wake utaathiri mwenendo wa kesi hiyo kwa kuwa maelezo yake hayakuwamo katika kifurushi cha comito hivyo washtakiwa hao hawakuyapata.

“…tunaomba pingamizi hili liangaliwe kwa uzito wake na kwa kuzingatia hayo yaliyosemwa na hatua ya kisheria iliyofikia tunasisitiza uwepo wa shahidi huyo uondolewe,” amedai Wakili Mtobesya.

Baada ya kutoa pingamizi hilo, Wakili Hilla aliibuka na kuipinga akiiomba mahakana hiyo itupilie mbali akidai hoja hiyo ilitakiwa kutolewa katika mahakama ya chini ambayo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kabla haijahamishiwa mahakamani hapo.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, alidai pingamizi hilo halina mashiko ya kisheria kwa kuwa lililetwa katikati ya ushahidi na kwamba walipaswa kuiibua mapema.

Wakili Kidando alidai, shahidi huyo aliorodheshwa tangu katika hatua ya awali na kwamba jina lake linasomeka namba 23 katika rekodi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Baada ya mapingamizi hayo, Jaji Tiganga aliamua kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo kwa muda wa dakika 15 kwa ajili ya kujipanga kutoa uamuzi.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake. Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!