August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika

Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa uamuzi dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na wabunge viti maalum 19, wakiongozwa na Halima Mdee, ya kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Shauri hilo limeahirishwa leo Jumatano, tarehe 6 Julai 2022, hadi Ijumaa ya tarehe 8 Julai mwaka huu baada ya Msajili wa Mahakama hiyo, Elimo Masawe, kusema uamuzi huo bado haujakamilika.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi kama inatoa kibali cha kufunguliwa kesi hiyo ya kina Mdee kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, au haitoi kibali cha kufunguliwa.

Tarehe ya kutolewa uamuzi huo ilipangwa na Jaji Mustafa Ismail, wiki iliyopita baada ya Mdee na wenzake 18, kuwasilisha hoja tano, wakiiomba mahakama ifanye mapitio ya kimahakama, juu ya mchakato uliotumika kuwafukuza uanachama wa Chadema.

Mawakili wa kina Mdee, wakiongozwa na Ipilinga Panya, walidai mchakato huo ulikuwa kinyume cha sheria.

Miongoni mwa hoja hizo Tano ni, maombi ya kuomba mapitio hayo yalifunguliwa ndani ya muda kisheria, wabunge hao kuwa na maslahi dhidi ya mchakato huo wakidai uliwaathiri kufuatia hatua ya Chadema kuwavua uanachama.

Nyingine ni, mchakato huo kuingiliwa na upendeleo kufuatia ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, waliowafukuza uanachama, kushiriki kikao Cha Baraza Kuu la Chadema, kilichotupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa.

Hoja nyingine ni maamuzi ya Chadema kuwafukuza uanachama kuwa ya umma na mwisho ikiwa wabunge hao kukosa nafasi ya kupata haki Yao ya kusikilizwa juu ya uamuzi huo.

Mbali na Chadema iliyoshtakiwa kupitia Bodi yake ya Wadhamini, wajibu maombi wengine katika shauri hilo ni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwansheria Mkuu wa Serikali (AG).

error: Content is protected !!