Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yamzua Lipumba kukomba ruzuku
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yamzua Lipumba kukomba ruzuku

Spread the love
PROF. Ibrahim Haruna Lipumba, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amegonga mwamba mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa Mbarala Maharagande, naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa CUF aliyekuwapo mahakamani hapo, ni kwamba jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa, wametupa maombi ya “timu Lipumba.”

Jopo la majaji hao liliongozwa na Jaji Mussa Kipenka. Majaji wengine, waliosikiliza shauri hilo, lilosajiliwa mahakamani hapo na kupewa Na.343/01/2018, ni Jaji Mziray na Jaji Ndika.

Maharagande anasema, mbali na kutupa maombi ya Lipumba, mahakama imemtaka mwanasiasa huyo kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Inayoitwa bodi ya wadhamini ya Lipumba, ilifungua shauri hilo katika mahakama ya rufaa, kupinga uamuzi wa mahakama kuu, kanda ya Dar es Salaam, uliozuia ruzuku ya chama hicho kukabidhiwa yeye na bodi yake feki.

Wadai katika shauri hilo, walikuwa Peter Michael Malebo, Thomas Malima na wajumbe wengine saba wa “bodi ya wadhamini ya Lipumba” ambayo pia  inatambuliwa na Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA).

Bodi ya Lipumba ilikwenda Mahakama ya Rufaa, kupinga maamuzi ya Jaji Wilfred Dyansobera, yaliyotolewa tarehe 29 Mei mwaka huu. Ilikuwa ni katika shauri Namba 80/2017.

Walalamikaji katika shauri hili, ni katibu wa bodi inayoungwa mkono na katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye ni mkurugenzi wa fedha wa chama hicho na kaimu katibu mkuu, Joran Lwehabura Bashange.

Katika shauri hilo, bodi ya Maalim Seif, imewashitaki mahakamani, Prof. Lipumba; Msajili wa Vyama, Jaji Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma maamuzi hayo, leo Jumatatu, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, ameeleza kuwa aombi ya Prof. Lipumba na washirika wake, yamekosa sifa kisheria na hivyo mahakama imeamua kuyatupilia mbali.

Majaji hao wanasema, “…Mahakama hii, inakubaliana na hoja za msingi za pingamizi la awali lililowekwa na mawakili wa utetezi, Daimu Halfani na Juma Nassoro, walioiwakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF katika shauri hilo… Mahakama imeyaondoa maombi hayo kwa gharama (Struck Out with Cost).

Mawakili wa watetezi – Juma Nassoro na Daimu Halfani – waliwasilisha hoja kadhaa za pingamizi (Preliminary Objections), kwa kunukuu maamuzi mbalimbali ya Mahakama Kuu za Tanzania, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki.

Miongoni mwa maamuzi hayo, ni pamoja na “Interlocutory Order/Decision” chini ya kifungu cha [Section 5(2) (d) Appellate Jurisdiction Act Cap 141 RE 2002 as amended by Act No. 25/2002] ambacho kisheria kinakataza kukatia rufaa au kuombewa kufanyiwa marejeo (Revision) na mahakama ya rufaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!