Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yamweka kizani mtoto wa Chacha Wangwe
Habari za Siasa

Mahakama yamweka kizani mtoto wa Chacha Wangwe

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imehalisha kutoa hukumu ya kesi inayomkabili, mtoto wa Marehemu Chacha Wangwe, Bob (25), ya upotoshaji kwenye Facebook kuhusu uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, anaandika Faki Sosi.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, ambaye amesema kuwa tayari ameshamaliza kuandaa hukumu hiyo na kwamba ataitoa tarehe 15 Novemba mwaka huu.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo upande wa jamhuri ulileta mahakamani hapo mashahidi sita huku upande wa utetezi shahidi alikuwa mmoja ambaye ni mshitakiwa mwenyewe.

Awali Bob alipandishwa kizimbani Mei 11, 2016 kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za upotoshaji kwenye akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Kwenye kesi hiyo namba 167 ya mwaka 2016 Bob Chacha Wangwe alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 15 mwaka 2016 na kwamba alichapicha maneno haya: “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!