Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yamwachia huru Mdee
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yamwachia huru Mdee

Halima Mdee (kushoto), akiwa na Ester Bulaya ndani ya jengo la mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuacha huru mbunge Viti Maalumu (asiyekuwa na chama), Halima James Mdee. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mdee alifikishwa mahakamani hapo na Jamhuri akituhumiwa kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Jamhuri, John Magufuli. Alidaiwa kutenda kosa hilo, tarehe 3 Julai 2017, alipokuwa mbunge wa Kawe, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alifukuzwa uanachama wa Chadema, yeye pamoja na wenzake 18, tarehe 27 Novemba mwaka jana.

Alituhumiwa kwa makosa usaliti, ikiwamo kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhujumu Chadema; kughushi nyaraka za chama hicho, kujipeleka bungeni na kujiapisha kuwa wabunge wa Viti Maalum, kinyume na maekelezo ya chama chenyewe.

Mpaka sasa, bado yuko bungeni kufuatilia, Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuendelea kung’ang’aniza kuwa bado wanachama wa chama hicho.

Halima Mdee (kushoto), akiwa na Ester Bulaya kwenye jengo la mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu

Uamuzi wa kumuachia huru Mdee, umetolewa na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba leo Alhamisi, tarehe 25 Februari 2021.

Akisoma uamuzu huo, Hakimu Simba amesema, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya Mdee.
Alisema, “…baada ya kupitia ushahidi wote, nimejitosheleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake. Hivyo, mshitakiwa nimeamua kumuachia huru.”

Mdee alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, tarehe 10 Julai mwaka 2017.

Mbunge huyo viti maalumu alidaiwa  kutenda kosa hilo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,  makao makuu ya Chadema, ambapo alidaiwa kusema, “Rais John Magufuli anaongea ovyo ovyo, anapaswa kufungwa breki.”

Katika utetezi wake, Mdee alidai kuwa maneno aliyodaiwa kuyasema hayaoneshi kama yalikuwa yanamlenga nani; na kudai kuwa mtu anayeongea ovyo ovyo maana yake, anaongea vitu ambavyo sio kweli na havina mantiki.

Mdee amefika mahakamani hapo akiwa na swahiba wake mkuu, Ester Bulaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!