Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yaipiga ‘stop’ Bodi ya Prof. Lipumba
Habari za Siasa

Mahakama yaipiga ‘stop’ Bodi ya Prof. Lipumba

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lilowekwa na mawakili wa Professa Ibrahim Lipumba la kuhusu kuzuwazuia wajumbe wake wa Bodi ya Wadhamini isifanye kazi mpaka shauri la msingi litakapo sikilizwa, anaandika Faki Sosi.

Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji Wilfred Dynasobera na kwamba bodi hiyo haitakuwa halali mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa.

Prof. Lipumba ambaye Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili vya Vyama vya Siasa ndiye aliyeunda bodi hiyo pamoja na kuwepo kwa mgogoro ndani ya chama hicho.

Mawakili wa upande wa Chama Cha Wananchi (CUF) wanamuunga Mkono Katibu Mkuu Maalimu Seif Sharif Ahmad ni pamoja na Fatma Karume na Mpoki Kabe. Upande wa Walalamikiwa ni Pamoja na Mashaka Ngole na Majura Magafu.

Kwenye kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2013 muombaji ni Ally Salehe Mbunge wa Malindi kwa tiketi ya CUF ambaye amishitaki bodi ya CUF iliyondwa na Prof. Lipumba pamoja na Rita.

Kesi ya Msingi itaendelea kusikilizwa kwa njia maandishi huko bodi ya Lipumba ikiwa haiwezi kufanya kazi kwa katazo la mahakama.

Hoja za muuombaji zitawasilishwa mahakamani hapo tarehe 27 Oktoba, mwaka huu, huku walalamikiwa wanatakiwa kujibu  Novemba 6, mwaka huu.

Hii hapa taarifa kamili ya hukumu hiyo iliyotolewa jana

CUF YASHINDA PINGAMIZI DHIDI YA LIPUMBA NA GENGE LAKE KESI YA BODI YA WADHAMINI-RITA:

TAARIFA RASMI YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) KUTOKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA-DAR ES SALAAM:

TAARIFA KWA UMMA

LEO TAREHE 5 OKTOBA, 2017 Mbele ya MHESHIMIWA JAJI WILFRED DYANSOBERA imetoa maamuzi (Ruling) juu ya Mapingamizi yaliyowekwa na Lipumba [aliyewakilishwa na Wakili Mashaka Ngole na Majura Magafu] na washirika wake wengine akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Shauri Namba Miscilleneous Civil Application No. 51/2017 kuhusu CUF kuomba kuwazuia Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyosajiliwa na Lipumba wasifanye kazi ya Bodi hiyo mpaka pale shauri la msingi Namba 13/2017 litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu. Mhe.Jaji ameyatupilia mbali mapingamizi hayo kutokana na kutokuwa na hoja za msingi za kisheria. Mhe Jaji amekubalia na Hoja zilizowasilishwa na Mawakili wasomi Mhe Fatma Karume, na Mhe. Mpoki Kabe. Maamuzi hayo yanatoa nafasi ya kwenda kusikilizwa undani wa Hoja zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Ally Salehe [Muombaji/Applicant]. Imekubaliwa kuwa hoja za pande zote mbili zitawasilishwa kwa maandishi [Written Submission] kwa utaratibu Mpaka Tarehe 19/10/2017 Ally Salehe awe amewasilisha na Tarehe 27/10/2017 walalamikiwa wawe wamejibu (Counter Affidavit) na Tarehe 6/11/2017 Ally Salehe awasilishe majibu zaidi (Rejoinder) na Tarehe 7/11/2017 inatajwa kwa kupagwa siku ya kutolewa Maamuzi.

USHINDI MWENGINE:
Shauri Namba 75/2017 Mwanasheria mkuu wa Serikali alifungua shauri hilo kwa lengo la kuomba kibali cha kukatia Rufaa (Application For Leave to Appeal) Maamuzi yaliyowapa ushindi hapo awali ya Shauri Namba 21/2017 kuhusu Ruzuku. AG ameeleza kuwa hawana nia ya kuendelea na shauri hilo. Lakini kutokana na kuwa tayari Upande wa CUF kupitia Mawakili Wasomi Mhe Juma Nassoro na Mhe Halfani Daimu kuweka Pingamizi la kisheria kwa kukosewa kwa vifungu vya sheria vilivyowekwa (Wrong Citation of provision of Law) shauri hilo likasikilizwa kwa maana ya kutambua kuwa AG amekubaliana na hoja hizo (Concede) na Mhe Jaji Ndyansobera ameliondoa shauri hilo Mahakamani (Struck Out).

SHAURI LA MADAI MISCELLENEOUS CIVIL CAUSE NO. 21/2017 KATI YA WABUNGE 19 DHIDI YA LIPUMBA:-
Shauri linasimamiwa na Mawakili Wasomi Mhe Mohamed Tibanyendera na Mhe. Hashimu Mziray tayari wahusika wote wameshapatiwa nyaraka husika na kuweka utaratibu uwasilishaji wa majibu (Counter Affidavit) mpaka Tarehe 19/10/2017 na Majibu (Reply to Counter Affidavit) Tarehe 27/10/2017 na Tarehe 31/10/2017 itatajwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa. Kwa mujibu wa sheria kutolewa KIBALI [LEAVE] ya kufunguliwa shauri hili mahakamani kisheria ni sawa na Zuio[INJUCTION] kwa mlalamikiwa. MAHAKAMA IMESHATOA KIBALI CHA KUWALINDA WABUNGE KUTOBUGHUDHIWA NA YEYOTE MPAKA HAPO SHAURI LA MSINGI LITAKAPOSIKILIZWA NA KUAMULIWA.[UNDER PROVISION CONNECTED BY PROHIBITION, CENTIORARY, AND MANDUMUS] HAKUNA MBUNGE ANAYEWEZA KUFUKUZIKA TENA KWA SASA.

MAPINGAMIZI[PRELIMINARY OBJECTIONS];

Pingamizi ni hatua ya kisheria ya kutaka kuiomba mahakama isisikilize kesi/shauri lililowasilishwa kutokana na sababu za nukta za kisheria [points of law]. Lipumba na kundi lake Tangu awali huu ndio umekuwa utaratibu anaotumia kupoteza muda na matokeo yake kuifanya Mahakama isifike mwisho wa Mashauri haya. Mhe. Joran Bashange –Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF ambaye pia ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara amesema “MSIMAMO WA CHAMA TANGU TUNAKUJA MAHAKAMANI TULIAMINI KUWA MAHAKAMA NDIO NJIA PEKEE INAYOWEZA KULIPATIA UFUMBUZI/KULITATUA SUALA HILI KWA MISINGI YA SHERIA NA HAKI …NA BADO IMANI YETU MBELE YA MAHAKAMA NI KUBWA NA IPO PALEPALE. WANACHAMA WASIWE NA HOFU SISI AMBAO WAMETUWEKA MBELE KULISIMAMIA SUALA HILI TUNALISIMAMIA NA MUDA MFUPI UJAO WATAONA MAJAWABU YA HILI TUNALOLISIMAMIA……” LIPUMBA NA GENGE LAKE WAACHE KUWEWESEKA NA KUTAFUTA VISINGIZIO….WAACHE MASHAURI YAMSINGI YASIKILIZWE MAHAKAMA IAMUE.

AIDHA, Mashauri mengine yote takribani 6 yameekewa utaratibu wa kutajwa na au kusikilizwa mpaka ifikapo Tarehe 31/10/2017 Mashauri hayo ni kama ifuatavyo;

1. Na.28/2017(Zuio la Ruzuku) kusikilizwa Tarehe 31/10/2017
2. Na.68/2017( kesi ya msingi ya Ruzuku) kusikilizwa Tarehe 31/10/2017
3. Shauri la Msingi Madai (Civil Case No. 13/2017) linahusu uhalali wa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF iliyosajiliwa na RITA- Ally Salehe dhidi ya Lipumba na wenzake. AG ameomba kuongezewa muda wa kuwasilisha majibu (Rejoinder) na kupewa mpaka Tarehe 11/10/2017 na Tarehe 31/10/2017 maamuzi yanatolewa.
4. Shauri la Jinai namba 50/2017 (Contempt of Court Proceedings)-shauri hili dhidi ya Lipumba na wenzake, Emmy Hudson-RITA, Franscis Mutungi linahusiana na kughushi nyaraka na kutaka kuingilia mwenendo wa mashauri yaliyopo mahakamani. Wakili Msomi Mhe Hashimu Mziray amewasilisha Pingamizi la kumtaka AG asiwatete MUtungi na Emmy Hudson kwa kuwa Shauri hili linawahusu wao binafsi na si kwa nafasi zao. Hoja zitawasilishwa kwa maandishi Wakili hashimu atawasilisha Tarehe 19/10/2017, AG atajibu Tarehe 23/10/2017 na Wakili Hashimu atawasilisha majibu ziada (Rejoinder) Tarehe 27/10/2017 na Tarehe 31/10/2017 Mhe Jaji atatoa Maamuzi (Ruling)
5. Na.80/2017 (maombi mapya ya Zuio la Ruzuku) Tarehe 19/10/2017 AG awasilishe majibu (Counter Affidavit) na Tarehe 27/10/2017 Bodi Halali ya Wadhamini -CUF kupitia Mawakili wake watawasilisha majibu (Reply to Counter Affidavit) na Tarehe 31/10/2017 inatajwa kwa kusikilizwa. .

TUNAWAPONGEZA WANACHAMA, MADIWANI NA WABUNGE WOTE WALIOJITOKEZA LEO KUHUDHURIA MAHAKAMANI. TUNAAMINI NA HIVYO NDIVYO ITAKAVYOKUWA KWAMBA HAKI ITAISHINDA BATILI.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 05/10/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

SALIM BIMANI
MKURUGENZI
Zantel +255 777 414112 / Tigo +255 655 314112

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
Phone No. 062577 TIGO CODE-+255 715 / ZANTEL CODE – +255 773 / VODA CODE- +255 767
maharagande@gmail.com

AG=ATTORNEY GENERAL /MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.

WAJUMBE WA BODI FEKI YA WADHAMINI YA LIPUMBA, WANAOTAKIWA KUZUILIWA NA MAHAKAMA KUFANYA SHUGHULI ZA BODI NI 1. PETER MALEBO, 2. THOMAS MALIMA, 3. HAJIRA SILIA, 4. AZIZI DANGESH,5. AMINA MSHAMU, 6. ABDUL MAGOMBA, 7. ASHA SULEIMANI, 8. SALHA MOHAMED, 9. SULEIMAN ISSA, NA 10. MUSA HAJI KOMBO.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!