October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yaigeukia Serikali kesi ya kina Kitilya

Spread the love

MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa Jamhuri kuharakakisha upelelezi wa kesi inayomkabili Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili wanaokabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Huruma shahahi Hakimu Mkuu katika Mahakama hiyo ameutaka upande huo mara baada ya Wakili wa Serikali Mkuu Kishenyi Mutalemwa kudai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kuifika ukingoni kukamilika.

Washatakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni pamoja na Shose Sinare aliyekuwa Miss Tanzania (1996) na Ofisa wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon.

Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alihoji ni ukingo gani huo ambao unazungumziwa na upande wa mashtaka.

Hakimu shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 30, mwaka huu na kuusisitiza upande wa mashtaka kufanya jitihada kukamilisha upelelezi.

Washtakiwa hao kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha ambapo Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd.

error: Content is protected !!