April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yagoma kuitwa idara

Spread the love

MAHAKAMA ya Tanzania, imepiga marufuku kuitwa idira na kwamba ni mhimili pekee unaojitegemea. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Onyo hilo limetumwa leo tarehe 30 Julai 2019, kwa vyombo ya habari na Nurdin Ndimbe, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania.

Ndimbe amesema, wanahabari wamekuwa wakitumia neno idara kwenye taarifa zao jambo ambalo si sahihi.

“Kwa barua hii, tunaomba kuanzia sasa katika taarifa zenu msitaje tena mahakama kama idara bali itambulike kama Mahakama ya Tanzania kama ilivyo Bunge la Tanzania,” amesema Ndimbe.

Amesema, kwa mujibu wa fungu la 107 A(1) na 107 (B) la Katiba wa Jamhuri ya Tanzania,  Mahakama ni mhimuli  wa dola kama ilivyo Bunge na Serikali.

error: Content is protected !!