Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mahakama yabatilisha hukumu ya Bob Chaha Wangwe
Habari Mchanganyiko

Mahakama yabatilisha hukumu ya Bob Chaha Wangwe

Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam imebatilisha hukumu ya mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wange- Bob Chacha Wangwe. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtaka Bob Chacha Wangwe kutakiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na miezi sita jela au faini ya Sh. 5 Milioni. 

Huruma Shahidi, Hakimu Mkazi Mkuu alitoa hukumu hiyo tarehe 15 Novemba mwaka 2017 ambapo mahakama hiyo ilieleza kuwa, imemtia hatiani Bob kwa makosa ya kutumia vibaya mtandao.

Awali, Bob aliyepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kushitakiwa kwa kesi namba 167 ya mwaka 2016  ya uchochezi ambapo alidaiwa  terehe 15 Machi mwaka 2016  alichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook maneno yafuatayo;

“Tanzania ni  nchi ambayo inajaza chuki wananchi ….matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe … haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwa sababu za kijinga.”

Leo  Mahakama Kuu mbele ya Jaji Seif Kulita imetoa uamizi wa kubatilisha na kufuta adhabu aliyopewa na Mahakama ya Kisutu.

Jebra Kambole, aliyemuwakilisha Bob mahakamani hapo aliwasilisha hoja tatu za kupinga hukumu hiyo ikiwa ni pamoja na kwamba, shitaka lilikuwa linashaka ambazo zilishindwa kuthibitika.

Pia uamuzi wa kumtia hatiani Bob ulitokana na upungufu wa utetezi wake na sio uzito wa uendeshaji mashtaka mwisho upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kuwa Bob alikiuka kifungu cha 16 cha makosa ya mitandaoni kwa kutopeleka vithibitisho vyote mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!