August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yabariki Mbowe kufukuzwa

Wafanyakazi wa Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima wakishuhudia vitu vyao vikitolewa nje siku chache zilizopita

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Ardhi imetupilia mbali maombi ya mfanyabiashara na mwanasiasa, Freeman Mbowe kutaka kurudishwa katika jengo la Bilicanas kwa madai kuwa aliondolewa bila ya utaratibu wa kisheria kufuatwa,anaandika Aisha Amran.

“Mahakama imejiridhisha kwamba NHC ilifuata taratibu zote katika kuiondoa Mbowe Hotels Limited, kupitia  ilani ya siku 30 iliyotolewa mara mbili na baadaye siku 14,” amesema.

Hapo awali kupitia mawakili wake, Mbowe alidai kuwa hakupewa ilani (notice) inayomtaarifu kuwa anapaswa kuondoka katika jengo hilo na kwamba aliondolewa bila kuwapo kwa amri ya mahakama na hivyo kutaka arudishiwe mali zake zote zilizochukuliwa na NHC kupitia kampuni ya udalali ya Foster Auctioneers and General Traders.

Hata hivyo Jaji Mwangesi amesema baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi wa pande zote mbili imetupilia mbali maombi ya Mbowe kutaka kurudishwa mali zake kwani ni mdaiwa anayepaswa kulipa deni lake ndipo arejeshewe mali hizo.

Wakili wa NHC, Aliko Mwamanenge amewambia wanahabari kuwa, wanaishukuru mahakama kwa kutenda haki kutokana na uamuzi uliotolewa.

“Mahakama imekubali kwamba kila kitu kilichofanyika siku ya kutolewa kilifanyika kihalali, hivyo mali zake haziwezi kurudishwa kwa sababu hajalipa deni analodaiwa, hivyo hadi hapo atakapolipa deni hilo,” amesema.

Wakili John Mallya ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaomuwakilisha Mbowe amesema hawajaridhishwa na uamuzi huo na kwamba tayari wameomba nakala ya hukumu ili waweze kukata rufaa katikaMahakama ya Rufaa.

“Tumeomba kusifanyike jambo lolote katika jengo la Bilicanas hadi hapo Mahakama ya Rufaa itakapotoa uamuzi wake,” amesema.

Katika kesi hiyo Na. 722 ya 2016 Mbowe, akili huyo alibainisha kwamba Mbowe katika jengo hilo ni mpangaji na hata mkataba wa ushirikiano ambao unadaiwa umefanyika kwa sasa hauwezi kufanyakazi kwa kuwa ulishakwisha muda wake.

Katika madai ya msingi ya Mbowe, Wakili Kibatala alidai mteja wake siyo mpangaji katika jengo hilo, bali ni mbia ambaye anamiliki asilimia 75 katika uendeshaji wake huku NHC wakimiliki asilimia 25.

Msingi wa pili, Kibatala alisema hata kama Mbowe angekuwa anadaiwa kodi kama wanavyodai NHC, kuondolewa kwake kulifanywa bila kuzingatia sheria kwani hakukuwa na amri ya mahakama inayowapa wadaiwa nguvu ya kisheria ya kumwondoa.

Kwa upande mwingine, Mbowe kupitia hati ya kiapo alisema hadaiwi hata senti tano na NHC kama pango la jengo la Billcanas, na kwamba amekuwa akilipa tozo zote zinazotakiwa kwa mujibu wa mkataba baina yake na shirika hilo.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo aliyoiwasilisha mahakamani, mmiliki huyo wa Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd alisema kwa mujibu wa mkataba wa ubia wa pande hizo mbili, anapaswa kuwalipa NHC mapato ya jengo kila mwezi.

Katika hati hiyo, Mbowe alisema hadaiwi fedha yoyote kwani amekuwa akitekeleza matakwa hayo ya kimkataba kama yalivyosainiwa mwaka 1997, huku akiambatanisha ushahidi wa risiti ya fedha ambazo amekuwa akilipa.

error: Content is protected !!