May 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yaamuru Maua Sama, Sudi Brown kufikishwa mahamakani, Serikali yaufyata

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la Serikali kujibu kwa kiapo shauri la maombi ya dhamana kwa Msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama, Watangazaji Sudi Kadio maarufu kama Soudy Brown na Shaffih Dauda na wengine wanne. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza upande wa utetezi waliomba Mahakama uiamuru upande wa Jamhuri kuwafikisha Mahamani watuhumiwa hao.

“Ni ukweli usiopingika kwamba ombi limekuja kwa njia ya maandishi. Sheria inataka kama maombi yameletwa kwa njia ya maandishi na kiapo hivyo na majibu yatolewe kwa njia hiyo.

“Waombaji hawapo mahakamani leo na mahamaka haijaridhisha kuwa waombaji wapo mikono mwa Polisi,” amesema Hakimu Shahidi.

Hakimu Shahidi amesema kuwa kiapo cha upande wa Jamhuri kifike mahakamani hapo kesho tarehe 25 na usikilizwaji kesho kutwa tarehe 26 na waombaji waje kutoka huko walipohifadhiwa.

Maua Sama na Soud Brown walishikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam tangu Jumapili ya tarehe 16 Septemba mwaka huu, kwa tuhuma za kudhalilisha fedha ya Tanzania.

Wengine Shafii Dauda, mtangazaji na mchambuzi wa soka, Anthony Luvanda (MC Luvanda), Michael Mlingwa, Fadhili Kondo na Benedict Felix Kadege wakishikiliwa kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa YouTube pasipo kusajili katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ombi hilo namba 13 la Mwaka 2018 liliwasilishwa na Wakili wa upande wa waombaji Jebra Kambole. Kambole aliwasilisha maombi ya kutaka dhamana ya watuhumiwa hao tarehe 21 Septemba Mwaka huu.

Ombi hilo liliwashtaki Mkuu wa Jeshi la Polsi, Mkurugenzi wa Uplelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Upande wa Jamhuri uliowakilishwa na wakili wa Serikali Tumaini Kweka amejibu hoja za upande wa waombaji kuwa hoja zao zimewasilishwa kwa njia ya maandishi nao wataji kwa njia ya maandishi kama yalivyomatakwa ya kisheria.

Kweka amesema kuwa waombaji waliwasilisha maombi kwa njia ya kiapo nao watajibu maomni hayo kwa njia hiyo.

Hata hivyo Kweka ameleza kuwa nakala ya maombi hayo ilichelewa kuwafikia ambapo ilifika saa 9 alasiri siku ya Ijumaa ya tarehe 21 Septemba ambapo kwa utaratibu wa Serika Ofisi zake hufungwa saa 9 na nusu.

Wakati shauri likiendelea majira ya saa 5 :45 na saa 6 kamili Jeshi la Polisi limewafikisha watuhumiwa hao mahakamani muda wowote kuanzia sasa watapandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yao.

error: Content is protected !!