Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama ya Ulaya yaihusisha Urusi mauaji aliyekuwa jasusi wake
Kimataifa

Mahakama ya Ulaya yaihusisha Urusi mauaji aliyekuwa jasusi wake

Alexander Litvinenko
Spread the love

 

ALEXANDER Litvinenko, jasusi wa zamani wa Urusi, aliuawa kwa sumu na majasusi yaliyotumwa na taifa hilo, Mahamaka ya Haki za Binadamu ya Ulaya, imeeleza katika hukumu yake ya leo Jumanne. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Litvinenko, aliuawa mwaka 2006 jijini London, nchini Uingereza baada ya kupewa sumu na majasusi wenzake wawili, waliotumwa na serikali ya Rais Vladimir Putin.

Hata hivyo, Urusi yenyewe imekana madai hayo na kuita hukumu hiyo kuwa ya kisiasa.

Katika uamuzi wake wa leo Jumanne – tarehe 21 Septemba – mahakama hiyo ya juu kabisa barani Ulaya imesema, imeweza kuthibitisha pasina shaka kwamba mauaji hayo yalifanywa na raia wawili wa Kirusi, Andrei Lugovoi na Dmitry Kovtun.

Uamuzi wa mahakama unatokana na shauri lililofunguliwa na kizuka wa Litvinenko, Marina, ambaye aliitaka mahakama hiyo kuchunguza na kumtangaza muhusika mkuu wa mauaji ya mumewe.

Majasusi hao wawili walisafiri kutoka Urusi hadi mji mkuu wa Uingereza, London, kwa dhamira ya kumuuwa jasusi mwenzao wa zamani, imesema mahakama hiyo katika hukumu yake.

“Operesheni hiyo changamano ilipangwa ikihusisha ununuwaji wa sumu kali na adimu sana kupatikana, mipango ya usafiri ya wawili hawa, na majaribio kadhaa na endelevu kuhusu sumu hiyo, yote yanaashiria kwamba Bwana Litvinenko alikuwa ndiye mlengwa,” ilieleza mahakama.

Alexander Litvinenko

Lugovoi, ambaye sasa ni mbunge nchini Urusi, na mfanyabiashara Kovtun walitambuliwa na polisi nchini Uingereza kama washukiwa wakuu baada ya wote wawili kukutana na Litvinenko katika hoteli moja iliyopo katikati ya London.

Liitvinenko alifariki dunia baada ya kunywa chai iliyochanganywa na mionzi ya sumu aina ya Polonium 210 kwenye hoteli hiyo, katika mkasa ambao tangu hapo umeyaathiri sana mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo, majaribio kadhaa ya kuwasafirisha watuhumiwa hao kutoka Urusi hadi Uingereza kukabiliana na kesi dhidi yao yalishindikana, na wote wamekanusha mashitaka yaliyokuwa yanawakabili, huku Lugovoi akidai pia kutumia kinga yake ya kibunge.

Kabla ya kifo chake, Litvinenko alitoa ujumbe akimshutumu Rais Putin kwa kumtilia sumu.

Wapinzani wa Putin wanayachukulia mauaji hayo kuwa ya kwanza kwenye orodha ndefu ya hujuma za Kremlin dhidi ya wakosoaji wake.

Hata hivyo, msemaji wa Putin, Dmitry Peskov ameutupilia mbali uamuzi wa leo wa Mahakama ya Haki za Binaadamu ya Ulaya, akisema, hauna mashiko yoyote ya maana.

Alisema, “bado hakuna matokeo ya uchunguzi, kwa hivyo kutoa kauli kama hizo hakuna mashiko yoyote. Hatuko tayari kukubaliana na uamuzi huu.”

Wakati hayo yakijiri, polisi nchini Uingereza, imetangaza muda mfupi uliyopita, kwamba ina ushahidi wa kutosha wa kuwashitaki raia watatu wa Kirusi kwa kumshambulia kwa sumu aina ya Novichok, jasusi mwengine wa zamani, Sergei Skripal, na binti yake, Yulia, katika mji wa Salisbury, mwaka 2018.

Wapelelezi wa kikosi cha kupambana na ugaidi walisema, waendesha mashitaka wamepitia upya ushahidi dhidi ya mtu aliyetambuliwa kwa jina la Sergey Fedotov, kwa ajili ya kumfungulia mashitaka ya mauaji, jaribio la mauaji, kusababisha madhara mwilini, na kumiliki na kutumia silaha ya kemikali.

Kama ilivyokuwa kwa Litvinenko, jasusi huyo wa zamani wa KGB naye alimtuhumu moja kwa moja Rais Putin kwa mashambulizi hayo, katika barua iliyosomwa hadharani baada ya kifo chake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!