July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama ya Misri yamuhukumu Morsi kunyongwa

Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Morsi akiwa gerezani alipohukumiwa kifungo cha miaka 20

Spread the love

ALIYEKUWA Rais wa Misri, Mohammed Morsi amehukumiwa kunyongwa mpaka kufa na Mahakama moja nchini Misri baada ya kukutwa na hatia.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, Mahakama hiyo ilimpata na hatia Morsi kufuatia kuvunjwa kwa magereza mwaka wa 2011.

Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.

Morsi aling’olewa madarakani na jeshi Julai, 2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake.

Kuanzia hapo chama chake cha The Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku huku mamia ya maelfu ya wafuasi wake kukamatwa na vyombo vya dola.

Kufuatia uamuzi huo wa kifo, sasa kauli nzima na ruhusa itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye sasa ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi ataonja mauti au la.

Sheria za nchi hiyo hata hivyo zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.

Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.

Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa ofisini.

error: Content is protected !!