April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Mtwara yamwachia huru Mwambe

Spread the love

MAHAKAMA ya Mkoa wa Mtwara leo tarehe 30 Aprili, 2020, imemwachia huru aliyekuwa Mbunge wa Ndanda kwa tiketi ya Chadema, Cecil Mwambe katika kesi ya uchochezi namba 263 ya mwaka 2017 iliyokuwa inamkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Katika kesi hiyo Mwambe alishitakiwa kwa makosa mawili, kosa la kwanza, kutoa kauli za uchochezi alizotoa katika Kata Reli, wilaya Masasi, huku kosa la pili ni kufanya njama ya kutaka kutenda ovu.

Hakimu Kabate R. ametoa uamuzi huo wa kumwachia huru Mwambe, baada ya upande wa mashataka kushindwa kuthibitisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo, ambayo pia hayakuleta athari yoyote kwa jamii husika.

Mwambe alifunguliwa kesi hiyo akiwa Mbunge wa Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lakini alijivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

error: Content is protected !!