Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama Kuu yawatosa Mbowe, vigogo wa Chadema
Habari za Siasa

Mahakama Kuu yawatosa Mbowe, vigogo wa Chadema

Spread the love

MAOMBI ya Rufaa ya viongozi wa chama cha Chadema yametupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa kutokana na hati ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa kutokuwa na sifa za kuwepo mahakamani. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe walikata rufaa wakiiomba Mahakama Kuu iitishe jalada la kesi yao ya jinai kwa ajili ya kuchunguza na kujiridhisha kuhusu usahihi na uhalali wa mwenendo wa amri mbalimbali zilizotolewa na mahakama kuhusu kesi hiyo.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imetupilia mbali rufaa hiyo kutokana na kuwepo kwa kasoro za kikanuni kwenye hati ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Eddy Fussi ndiye aliyesoma uamuzi huo leo tarehe 5 Oktoba 2018, ulioandaliwa na Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa waliosoma uamuzi huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jopo, Shaban Lila na Jacobs Mwambegele.

Kwa mujibu wa Naibu Msajili Fussi, taarifa ya kusudio la kukata rufaa haikubainisha kiini cha uamuzi na au amri ya Mahakama Kuu waliyokuwa wakiukatia rufaa.

Viongozi hao wa Chadema walikata rufaa wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupilia mbali maombi ya mapitio ya mwenendo wa kesi yao ya msingi ya jinai, uliotolewa na Jaji Rehena Sameji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!