May 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Kuu yamtoa gerezani Lulu

Elizabeth Michael 'Lulu'

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imembadilishia kifungo Msanii wa Filamu, Elizabeth Micheal ‘Lulu’ kutoka kwenye kifungo cha Magereza na kutumikia kifungo cha nje. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lulu aliachiwa Mei 12 mwaka huu majira ya saa 2:30 asubuhi na kuanza kutumikia adhabu hiyo akiwa nje ya gereza.

Novemba 13 mwaka 2017 Lulu alihukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Sam Rumanyika baada ya kusikiliza ushahidi wa utetezi na ule wa Jamhuri.

Jeshi la Magereza limethibitisha kupokea amri ya mabadiliko adhabu ya msanii huyo ambapo atatolewa kutoka magereza na ataanza utaratibu wa adhabu ya kifungo cha nje.

Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

error: Content is protected !!