July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Kuu yaamua mita 200

Spread the love

JOPO la Majaji watatu mahakama Kuu ya Dar es Salaam leo limetoa hukumu juu kesi iliyofunguliwa na Ammy Kibatala kupitia wakili Peter Kibatala kuhusu umbali wa mita 200 wa mwananchi kukaa baada ya kupiga kura iliyokuwa na mvutano kwa muda mrefu. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Kesi hiyo namba 37 ya mwaka huu, mlalamikaji anaoiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo

Jopo hilo la majaji linaongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo pamoja na Lugano Mwandambo na Aloysius Mjujulizi

Kesi hiyo ilishindwa kusikilizwa siku ya kwanza baada ya upande wa serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka pingamizi sababu walipokea notisi ya walalamikaji muda wa jioni hivyo hawakujiandaa hali iliyopelekea kesi hiyo kuahirisha.

Kabla Majaji hawajatolea uamuzi ombi hilo walimshauri Wakili wa mlalamikaji Peter Kibatala kubadilisha mashtaka na kumshtaki Mkurugenzi wa Uchaguzi kwani ndiye mtendaji mkuu wa tume ya taifa ya Uchaguzi badala ya Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuangalia katiba Ibara ya 74, kifungu kidogo cha 7, inayosomeka “Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.”

Baada ya marekebisho hayo, kesi hiyo iliyovutia watu wengi iliahirishwa mara mbili hadi ilipotolewa hukumu jana katika kesi hiyo, mgombea huyo ambaye pia ni mpiga kura mwenye maslahi na uchaguzi mkuu ujao, aliomba mahakama kwa mujibu wa kifungu hicho sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 ifafanue kuhusu haki za wapiga kura.

Mlalamikaji anaitaka mahakama iseme na kutafsiri kifungu hicho kinamaanisha nini kuhusu haki hiyo kufuatia kauli iliyotolewa na NEC, pamoja na Rais Jakaya Kikwete kwamba wananchi wakishapiga kura hawaruhusiwi kukaa eneo la vituo vya kupigia kura umbali wa mita 200.

Aidha, anaitaka mahakama itamke kama ni halali kwa Rais na Tume ya Uchaguzi (NEC) kuzuia wananchi kukaa kwa utulivu umbali huo ama la.

Kibatala kwa upande wake amesema hajaridhika na uamuzi uliotolewa na na majaji watatu wa Mahakama Kuu, hivyo amepanga kukata rufaa ili haki itendeke kwa maslahi ya chaguzi zitakazofuata, kwani kwa uchaguzi huu, muda umeshakwisha.

error: Content is protected !!