January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Kuu Marekani yaidhinisha ndoa ya jinsia moja

Waandamanaji wakipinga ndoa za jinsia moja

Spread the love

MAHAKAMA  Kuu nchini Marekani, imetoa uamuzi unaosema kwamba, kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Marekani, watu wenye jinsia zinazofanana kibaiolojia kama ilivyo kwa watu wenye jinsia tofauti kibaiolojia, wanayo haki ya kuoana. Anaandika  Deusdedit Kahangwa … (endelea).

Uamuzi huu unapingana moja kwa moja na msimamo rasmi wa Kanisa Katoliki Duniani ambalo linafundisha kwamba, kwa mujibu wa Biblia Takatifu, watu wenye jinsia zinazofanana kibaiolojia hawana haki ya kuoana. Kanisa Katoliki linafundisha kwamba ni watu wenye jinsia tofauti kibaiolojia pekee ndio wenye haki ya kuoana.

Mahakama Kuu ilitoa uamuzi huo mnamo 26 Juni 2015, ambapo majaji (5) kati ya tisa waliunga mkono hoja hiyo wakati majaji wanne (4) wakipinga. Hukumu hiyo, ilisomwa na Jaji Anthony Kennedy kwa niaba ya wenzake.

Hukumu hiyo imetokana na kesi ya “Obergefell vs. Hodges” ambapo walalamikaji waliiomba Mahakama hiyo  kutamka kwamba sheria zinazokataza ndoa za jinsia moja katika majimbo ya Ohio, Tennessee, Michigan and Kentucky ni batili hata hivyo, hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu inayagusa majimbo yote hamsini (50) ya Marekani.

Kwa hiyo, sheria zote zilizokuwa zinapiga marufuku ndoa za jinsia moja katika majimbo kumi na tatu (13) zimebatilishwa rasmi. Majimbo thelathini na saba (37) tayari yalikuwa yanaruhusu ndoa hizo. 

Sehemu ya hukumu hiyo inasomeka hivi: The nature of marriage is that, through its enduring bond, two persons together can find other freedoms, such as expression, intimacy, and spirituality. This is true for all persons, whatever their sexual orientation... The right of same-sex couples to marry that is part of the liberty promised by the Fourteenth Amendment is derived, too, from that Amendment’s guarantee of the equal protection of the laws.” Nakala ya hukumu nzima inapatikana hapa.    

Kwa mujibu wa Katekisimu ya Kanisa Katoliki ibara ya 1601, ndoa umefafanuliwa kama ifuatavyo: “ Marriage is a lifelong partnership of the whole of life, of mutual and exclusive fidelity, established by mutual consent between a man and a woman, and ordered towards the good of the spouses and the procreation of offspring.

Katekisimu hiyo hiyo, katika ibara ya 2366 inafafanua fundisho hili kwa kutamka yafuatayo: The Church, which is ‘on the side of life,’ teaches that ‘it is necessary that each and every marriage act remain ordered per se to the procreation of human life.’ ‘This particular doctrine, expounded on numerous occasions by the Magisterium, is based on the inseparable connection, established by God, which man on his own initiative may not break, between the unitive significance and the procreative significance which are both inherent to the marriage act.’

Hivyo basi, ni wazi kwamba Mahakama Kuu na Mamlaka Kuu ya Kanisa Katoliki Duniani yenye makao yake Makuu huko Vatican zimetofautiana. Wakati Kanisa Katoliki linasema ndoa ni taasisi kati ya watu wenye jinsia tofauti kibaiolojia, Mahakama Kuu inasema hata watu wenye jinsia moja wanayo haki ya kuoana.

Hii maana yake ni kwamba, nchini Marekani, fasili ya ndoa ya kidini ni tofauti na fasili ya ndoa ya kiserikali lakini, kwa kuwa Katiba ya Marekani inatambua ukuta unaotenganisha dini na serikali ni wazi kwamba viongozi wa dini mbalimbali nchini Marekani wanayo haki ya kuendeleza msimamo wao wa kukataa kufungisha ndoa za jinsia moja bila hofu kusumbuliwa na serikali ya nchi hiyo.

Kwa hiyo, kazi muhimu iliyo mbele ya viongozi hao wa kidini nchini Marekani ni kutoa elimu ya uraia kwa waumini wao kuhusu maana na umuhimu wa dhana ya kutenganishwa kwa dini na dola, kwa upande mmoja, na tofauti zilizopo kati ya ndoa za kidini na ndoa za kiserikali, kwa upande mwingine.

Jukumu hilo wanalo pia viongozi wa kidini katika mataifa mengine pia, ikiwemo Tanzania, ambako katika za nchi zinautambua ukuta unaotenganisha dini na dola.  

error: Content is protected !!