July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama kuamua hatima uchaguzi TFF leo

Wallace Karia, Rais wa TFF

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam nchini Tanzania, leo Ijumaa saa 6:00 mchana, itatoa hukumu ndogo ya ama kuzuia uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uendelee au iusimamishe. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya mawakili wa pande zote mbili, kuwasilisha hoja zao mbele ya Jaji.

Kesi hiyo ya kupinga uchaguzi huyo, imeyofunguliwa na Ally Saleh ‘Alberto’ ambaye alikuwa moja ya wagombea kwenye uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika tarehe 8 Agosti, 2021, jijini Tanga, ambapo mpaka sasa kamati ya uchaguzi imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais. Karia ni rais wa shirikisho hilo kwa sasa.

Kesi hiyo ya madai namba 98 ya mwaka 2021, iliyofunguliwa na Ally Salehe, raia wa Tanzania anayeishi Zanzibar ambayo itakuwa chini ya Jaji Kakolaki ambapo wadai ni TFF, Bodi ya wadhamini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

error: Content is protected !!