Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama Kenya yasema mchakato BBI haukufuata sheria
Kimataifa

Mahakama Kenya yasema mchakato BBI haukufuata sheria

Spread the love

 

Mahakama ya upeo nchini Kenya imesema kwamba mchakato mzima wa marekebisho ya katiba ulikiuka sheria na kwa hivyo si halali. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kulingana na uamuzi wa wengi katika mahakama hiyo msuada wa marekebisho ya katiba haukufuata kanuni na utaratibu wa sheria.

Akitoa uamuzi wake Jaji Njoki Ndung’u ambaye ndiye wa pekee aliyeunga mkono mchakato wa BBI alisema kuwa Rais Uhuru Kenyatta hakuanzisha mchakato wa marekebisho ya katiba, kupitia Mpango wa BBI.

Katika uamuzi wake, leo Alhamis tarehe 31 Machi 2022 Jaji Ndung’u hata hivyo ameeleza kuwa Rais anaweza kuanzisha mchakato huo kwa wadhifa wake binafsi au rasmi kwa vile amechaguliwa kidemokrasia na Wakenya.

“Nilisoma kwa makini maamuzi yote, nikitafuta sababu zinazofaa za uamuzi wa kumtenga Rais katika mchakato wa marekebisho na siwezi kupata maelezo yenye mantiki ya kikatiba,” amesema.

Amesema Wakenya wana haki ya kufurahia uwakilishi kutoka kwa viongozi wao waliochaguliwa kihalali, ambao kupitia kwao wanaweza kutumia mamlaka ya kujitawala.

Uamuzi wa mahakama ya upeo unazamisha kabisa matumaini ya kufufua mchakato wa BBI.
Katika uamuzi wake, majaji sita walikubaliana na mahakama kuu na ile ya rufaa kuharamisha mchakato huo.

Walisisitiza kwamba rais Uhuru Kenyatta hana uwezo wa kuasisi mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho katika nafasi yake kama kiongozi wa taifa.

Aidha, rais anaweza tu kusimamia mchakato huo kama mkenya wa kawaida tu.

Upande wa rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga, ulipewa afasi ya kuwasilisha rufaa katika vipengele saba vilivyotajwa na jaji mkuu Martha Koome.

Jaji mkuu Martha Koome alisema kwamba mahakama hiyo itatoa uamuzi kamili siku ya Jumanne wiki ijayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!