March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Kenya yamkubali Kenyatta

Spread the love

MAHAKAMA ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi mbili zilizowasilishwa kupinga uchaguzi wa marudio, imeidhinishwa ushindi wa Kenyatta.

Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi. Kesi ya Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.

“Uchaguzi wa 26 Oktoba mwaka huu uliendeshwa sawa na na ushindi wa Kenyatta ni sahihi.
Kila upande utasimamia gharama yake,” amesema.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais wa marudio akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.

Jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya wapiga kura milioni 19.6 ambao walijiandikisha walishiriki uchaguzi huo.
Mahakama ya juu nchini humo ilifuta uchaguzi uliofanyika Septemba mwaka huu na kuamuru uchaguzi urudiwe ambao ulifanyika Oktoba 26 mwaka huu.

Katika uchaguzi uliofutwa na mahakama aliyekuwa mgombea urais kupitia Muungano wa NASA, Raila Odinga alipata kura zaidi ya milioni sita huku Kenyatta akiibuka na zaidi ya kura milioni nane.

error: Content is protected !!