February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Kenya yaamuru mitambo ya tume ichunguzwe

Spread the love

MAHAKAMA Kuu nchini Kenya imekubali ombi la  Muungano wa Upinzani (NASA), nchini humo kukagua mitambo iliyotumiwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Agost 8 mwaka huu, anaandika Irene David.

Kesi hiyo imewasilishwa na NASA kupitia aliyekuwa mgombea wake urais, Raila Odinga, akipinga ushindi wa Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee.

Mahakama ya juu nchini humo, imetoa ruhusa kwa mawakili wa Raila  kuchunguza  mitambo iliyotumika kuhesabu kura .

Uchunguzi wa mitambo hiyo utaisaidia mahakama kutoa maamuzi yenye haki kwa pande zote ambapo ripoti hiyo ya uchunguzi inatarajiwa kukamilika hapo kesho.

Mpaka sasa bado Uhuru hajaapishwa mpaka kesi ya pingamizi la ushindi wake itakapo malizika.

error: Content is protected !!