Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Mahakama Kenya waonya wanahabari, mawakili
Makala & Uchambuzi

Mahakama Kenya waonya wanahabari, mawakili

Spread the love

MAHAKAMA ya juu nchini Kenya imewaonya wanahabari, mawakili na wahusika wengine wa kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya mpinzani wake, Raila Odinga, anaandika Victoria Chance.

Kenyatta ametangazwa mshindi wa kiti cha urais kupitia chama cha Jubilee huku aliyekuwa mgombea kupitia Muungano wa NASA, Raila Odinga akianguka katika uchaguzi huo na kukimbilia mahakamani.

Mahakama hiyo imewaonya watu wote wanaozungumzia kesi hiyo nje ya mahakama na kwamba masuala ya mahakama yatashughulikiwa na chombo hicho pekee.

Takribani wiki mbili sasa tangu uchaguzi wa Kenya kufanyika ambapo Uhuru Kenyatta (JUBILEE) aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Laila Odinga (NASA), huku nyuma ya pazia ikisemekana kuwa

Uhuru Kenyatta kapata ushindi kwa njia isiyo sahihi hivyo suala hilo kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya juu nchini Kenya.

Agizo hilo limetolewa na mahakama huku hatua mbalimbali za kesi hiyo zikiendelea ambapo mapema jumatano ya wiki hii mawakili watakaoiwakilisha Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) wanaoongozwa na Poul Nyamodi na Kamau Karori wamekabidhiwa nakala za stakabadhi zote za uchaguzi tayari kwa kujibu malalamiko na wale wa Uhuru Kenyatta kupitia kampuni ya uwakili ya Otachi na Ogeta wanatakiwa kuandaa majibu ya malalamiko.

Kesi hiyo inatarajiwa kushika kasi wiki ijayo baada ya kikao kitakachojadili jinsi ya kuishughulikia kesi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Lowassa: Mwanasiasa aliyetikisa CCM, Chadema

Spread the loveWAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!