June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama imeishuhudisha haki

Spread the love

KUFUNGULIWA kwa gazeti la MwanaHALISI kupitia hukumu ya mahakama kumetajwa kama hatua muhimu inayoongeza kitu katika dhana ya udumishaji wa uhuru wa kujieleza nchini. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC), Onesmo Olengurumwa ametoa msisitizo huo akizungumzia uamuzi wa Mahakama Kuu kupitia Jaji Salvatory Bongole kutoa amri ya kufunguliwa kwa gazeti hilo lililofungiwa Julai 30, 2012 umesaidia kurudisha imani ya wananchi kwa mahakama kuwa kumbe inaweza kutenda haki.

“Tunatoa pongezi kwa mahakama kuendelea kuonesha umuhimu wa kuwa na uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari kwa kuliachia huru gazeti la kiuchunguzi la MwanaHALISI,” amesema.

Amekumbusha kuwa Mtandao ulikuwa mstari wa mbele kushirikiana na asasi nyingine za kiraia kupinga uamuzi wa kufungiwa MwanaHALISI uliofanywa na Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Dk. Fenella Mukangara.

“Ikumbukwe Mtandao tulipinga kwa nguvu uamuzi ule kwa kuona ni kitendo cha matumizi mabaya ya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 iliyotumika kulifungia gazeti hili bila ya makosa,“ amesema Onesmo.

Waziri alifungia gazeti hilo kupitia Tangazo la Serikali Na. 258 la 27 Julai, 2012.

error: Content is protected !!