Mahakama ya Afrika Kusini imeamua rais wa zamani wa Taifa hilo, Jacob Zuma anapaswa kurejea gerezani, kwa sababu msamaha wa kimatibabu aliopewa awali ulikuwa “kinyume cha sheria.” Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).
Muda aliokaa nje ya gereza haupaswi kuhesabiwa katika hukumu yake ya miezi 15, mahakama ya Pretoria ameamua.
Zuma aliachiliwa huru tarehe 5 Septemba 2021, kwa hali ya kiafya ambayo haikufichuliwa.
Alikuwa amefungwa gerezani kwa kushindwa kuhudhuria uchunguzi kuhusiana na na ufisadi wakati wa urais wake.
Zuma mwenye umri wa miaka 79 alijisalimisha kwa polisi Julai 2021, lakini kifungo chake, ambacho hakikutarajiwa kiliibua maandamano na uporaji, maeneo mbalimbali nchini humo.
Zaidi ya watu 300, wengi wao wakiwa ni kutoka katika ngome ya Zuma ya jimbo la KwaZulu-Natal, walifariki dunia katika maandamano hayo ya ghasia.
Leave a comment