October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Afrika Kusini yaamuru ndege ya Tanzania iachwe huru

Spread the love

NDEGE ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), aina ya Air Bus A220-300 iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya mahakama, imeachwa huru. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 4 Septemba 2019 na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia ukurasa wake wa twitter.

Katika andiko lake, Dk. Abbasi amesema ndege hiyo imeachwa baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini kutoa hukumu katika kesi ya fidia iliyofunguliwa na mkulima Hermanus Steyn dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Dk. Abbasi ameeleza kuwa, katika hukumu hiyo, Mahakama ya Gauteng iliamuru ndege hiyo iachwe, pamoja na mlalamikaji kulipa gharama zilizotumika katika kuiendesha kesi hiyo.

“Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini leo imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe, na mlalamikaji alipe gharama za kesi. Tunawashukuru wote kwa uvumilivu,” ameandika Dk. Abbasi katika ukurasa wake wa Twitter.

Ndege ya ATCL ilishikiliwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo tarehe 23 Agosti mwaka huu, baada ya mahakama hiyo kutoa amri ya kuishikilia kutokana na kesi y a madai ya iliyofunguliwa na Steyn.

error: Content is protected !!