NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Uingereza Harry Maguire, Rahim Sterling na Kyle Walker wamejumuhishwa kwenye kikosi cha wachezaji 11 bora wa michuano ya Euro 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)
Michuano hiyo ambayo ilifikia ukingoni, tarehe 11 Julai 2021, kwa timu ya Taifa ya Italia kuibuka na ushindi wa penalti 3-2, dhidi ya Uingereza mara baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1.
Mara baada ya michuano hiyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), imetoa majina 11 ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha michuano hiyo na timu ya Taifa ya Italia ikiongoza kwa kutoa wachezaji watano.

Katika kikosi hiko lilikosekana jina la mfungaji bora wa michuano hiyo Cristiano Ronaldo ambaye alicheza michezo minne na kupachika mabao 5.
Wengine waliochaguliwa kwenye kikosi hiko ni mchezaji bora wa michuano hiyo na mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Italia, Donnarumma, Leornado Bonucci, Spinazolla.
Kwenye safu ya kiungo waliochaguliwa ni Jorginho, Pedro Gonzalez ‘Pedri’ na Pierre-Emile Hojbjerg, huku upande wa washambuliaji kukiwa na Romelu Lukaku pamoja na Federico Chiessa.
Leave a comment