JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania amesema, vitambulisho vya wajasirimali ‘machinga’ vitaboreshwa zaidi ili kuwawezesha kupata mikopo benki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Rais Magufuli amesema hayo wakati akihutubia na kuzindua Bunge la 12 leo Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020 jijini Dodoma.
Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, vitambulisho vya wajasirimali vilivyokuwa vinatolewa huko nyuma sasa vitaboreshwa zaidi kwa kuweka taarifa muhimu.
“Kwa miaka mitano ijayo, tutaviboresha ikiwemo kuweka picha na taarifa nyingine muhimu kama ilivyo kwenye vitambulisho vya taifa na paspoti.”

“Hii itawezesha wafanyabiashara watakaotumia vitambulisho hivyo kutambulika ikiwemo kwenye benki na hivyo kupata mikopo ili kukuza biashara zao,” amesema Rais Magufuli
Amesema, hatua hiyo “itawawezesha kukuwa na kutajirika, tunataka wafanyabiashara wadogo wadogo kukuwa na siyo kubaki walivyo”
Miongoni mwa wageni mbalimbali waliohudhulia ufunguzi huo ni Marais wastaafu wa Tanzania; Jakaya Mrisho Kikwete na Ali Hassan Mwinyi na makamu wa rais mstaafu; Ghalib Mohamed Bilal.
Pia, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Leave a comment