September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli, vigogo kushiriki ujenzi Ikulu Dodoma

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli kesho Jumamosi tarehe 30 Mei, 2020 atawaongoza marais wastaafu wa nchi hiyo, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Marais hao wastaafu ni; Ali Hassan Mwinyi wa awamu ya pili, Benjamini Mkapa aliyeongoza awamu ya pili na Jakaya Kikwete, awamu ya tatu.

Mama Maria Nyerere atahudhuria kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia tarehe 14 Oktoba 1999, London nchini Uingereza alikokwenda kwa matibabu.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa aliyoitoa leo Ijumaa tarehe 29 Mei, 2020 imesema shughuli hiyo itafanyika kesho kuanzia saa 3 asubuhi.

Leo, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa uwekaji wa jiwe hilo la msingi.

error: Content is protected !!