January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli: Tunajenga barabara si majambazi

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli

Spread the love

DAKTA John Magufuli-Waziri wa Ujenzi, amesema wizara yake inahusika zaidi na ujenzi wa barabara na sio kuzuia majambazi wanaojihusisha na utekaji wa magari. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Magufuli ametoa kauli hiyo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu (CCM), aliyetaka kujua ni hatua gani ambazo zinachukuliwa na wizara hiyo kutokana na kujitokeza vitendo vya utekaji wa mabasi.

Amesema kazi ya wizara yake ni kujenga barabara kwa kiwango bora na kwamba kuhusu ujambazi, wanahusika Wizara ya Mambo ya Ndani.

Awali, katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Al-Shaymaa Kwegyir (CCM), alitaka kujua kilichokwamisha kukamilika kwa barabara Bagamoyo-Msata na kujua ni lini itakamilika.

Pia mbunge huyo, alitaka kujua Serikali inawajibika vipi na hasara inayotokana na ucheleweshaji wa kukamilika kwa barabara hiyo pamoja na kutaka kujua ni kiasi gani cha fedha kimetumika mpaka sasa.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, amesema mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Bagamoyo-Msata yenye urefu wa kilometa 64, unatekelezwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa kilometa 60 na sasa umekamilika kwa asilimia 98.2.

Lwenge ameongeza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa ucheleweshwaji wowote wa barabara hiyo, hakuna hasara yoyote iliyojitokeza.

Aidha, amesema kuwa hadi ujenzi huo utakapokamilika kwa awamu zote mbili, utagharimu jumla ya Sh. 125.68 bilioni.

error: Content is protected !!