June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli: Nitarekebisha makosa ya watangulizi

Spread the love

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amesema, yapo makosa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tatu na ya nne na kwamba, anakwenda kuyapatia ufumbuzi. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Serikali ya Awamu ya Tatu iliongozwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambapo Serikali ya Awamu ya Nne na ambayo inaondoka madarakani imeendeshwa na Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za mgombea urais kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza Dk. Magufuli amesema, serikali hizo kuna baadhi ya mambo waliyochelewa kuyafanya na kusababisha nchi kufika hapa ilipo.

“Yapo yaliyofanywa na awamu zilizopita hayakwenda vizuri na mimi nakwenda kuyapatia ufumbuzi,” amesema Dk. Magufuli na kuongeza kwamba, atakapochaguliwa na wananchi ataboresha maisha.

Amesema kuwa, wakati akizunguka mikao mbalimbali aligundua kuwepo kwa kero mbalimbali licha kuwa maji ndio kero kubwa ya Watanzania.

“Nashukuru kuwa awamu ya nne imetimiza suala la umeme, tutachimba mabwawa na tutahakikisha kuwa vyote vinapatikana sambamba,” amesema Dk. Magufuli.

Pia amepongeza ulinzi na usalama na kwamba Jeshi la Polisi, Mgambo , Zima Moto wataongezewa mishahara.

“Nitaiboreshe kwani mimi nitakuwa amiri jeshi mkuu aliye komaa ambaye naweza kupiga push up,” amejigamba Magufuli.

Amezungumzia Muungano wa Tanzania kuwa hatawavumilia watu wanaotaka kuuvunja. “Nitalala naye mbele kwa mbele mtu atakayeuchezea muungano, lazima muungano tuudumishe.”

Mwenyekiti wa chama hicho, Dk. Kikwete amesema kuwa katika kuteua wagombea, wamezingatia suala la afya zaona kwamba, wamemethibitisha kuwa Dk. Magufuli ndiye aliyeonekana kuwa bora.

Rais kikwete ametoa onyo kwa mtu yoyote atakaye fanya vurugu wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo kwani “mtu asiyejipenda afanye uhuni kesho, mimi ndio amri jeshi mkuu.”

error: Content is protected !!