May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Magufuli ni muoga’

John Magufuli, Rais wa Tanzania

Spread the love

UTETEZI wa Rais John Magufuli juu ya hatua ya vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kufanyika Ikulu katika makazi na ofisi ya rais umepingwa huku mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho yakitajwa kama “uoga wa kukosolewa,” anaandika Pendo Omary.

Vikao vya CCM vilivyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ni kikao cha Kamati Kuu (CC) yenye wajumbe 34 na Halmashauri Kuu (NEC) yenye wajumbe zaidi ya 380.

Rais Magufuli alinukuliwa akisema “Kama kuna vyama vingine vinataka kuja kufanyia mikutano hapa (Ikulu), basi vinakaribishwa ili mradi waombe na utaratibu wa hapa unajulikana kwamba ni lazima tujue ajenda zao na tusikilize wanayozungumza.”

Rais Magufuli alisisitiza kuwa haitakuwa mara ya mwisho kufanyia mikutano ya CCM Ikulu na hakuna atakayempangia afanye mkutano wapi. Alikuwa akijibu malalamiko ya wananchi mbalimbali waliokosoa hatua ya mikutano hiyo ya CCM kufanyika Ikulu.

Akitoa maoni yake kuhusu suala hilo Juju Danda, Katibu Mkuu wa chama cha NCCR- Mageuzi amesema “hayo ni maneno ya kujikosha. Sisi wapinzani hatuwezi kufanya vikao Ikulu pamoja na Mwenyekiti wa CCM huo ni muendelezo wa rais kutumia madaraka yake vibaya.”

Danda amesema wana CCM wamekuwa wakishangilia vitendo vya Rais Mgufuli kuwaminya wapinzani lakini sasa amewageukia wana CCM kwa kuanza kuwapunguza katika vikao vya maamuzi ili awadhibiti kiurahisi.

“Tunawapa CCM pole sana. Nia ya Rais Magufuli ni kuhakikisha hakosolewi. Hata hatua yake ya kupunguza wajumbe wa Halmashauri Kuu ni katika kuhakikisha anabaki na watu wachache ambao watafanya atakavyo,” amesema Danda.

error: Content is protected !!