January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli ndiye rais wa awamu ya tano wa Tanzania

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza rasmi Dk. John Pombe Magufuli, kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo wagombea wanane walikuwa kwenye kinyanyiro hicho. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye ukumbi Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam amedai kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa uhuru, haki na uwazi na matokeo hayo ndio maamuzi ya watanzania.

Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametangazwa kuwa rais kwa kupata idadi ya kura 8,882,935 ambayo ni sawa na asilimia 58.46.

Kwa kujibu wa Jaji Lubuva, mgombea wa Chadema, Edward Lowassa amepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97 na aliyeshika nafasi ya tatu ni Anna Elisha Mngwira wa ACT aliyepata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65.

Wengine ni Chief Lutalosa Yemba wa ADC aliyepata kura 66,049 sawa na asilimia 0.43 akifuatiwa na Hashim Rungwe Spunda wa Chaumma aliyepata kura 49,256 sawa na asilimia 0.32.
Wagombea wa vyama vilivyosalia vya NRA kura 8,028,TLP kura 8,198 na UPDP kura 7,785 wote wakipata asilimia 0.5.

Hata hivyo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imefuta uchaguzi wa visiwani humo mpaka siku 90 baadaye kutokana na udhaifu wa Tume hiyo ambako wenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salim Jecha amekiri kuwepo kwa dosari hizo.

error: Content is protected !!