KIFO cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi klilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 2 Mei 2019, kimeshtua wengi ikiwemo Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Watu wa kada mbalimbali wameonesha kuguswa na msiba huo mzito kwa taifa, huku wengi wao wakieleza kwamba tasnia ya sekta binafsi imekosa pigo kutokana na mchango wa Dk. Mengi aliokuwa akiutoa katika sekta hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ameonesha kusikitishwa na kifo cha Dk. Mengi akiandika kuwa, ataukumbuka kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa.
“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo ktk kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara,” ameandika Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter.
https://twitter.com/MagufuliJP/status/1123809850096537600
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa Twitter ameonesha kusikitishwa na kifo cha Dk. Mengia akisema kwmaba atamkumbuka kwa mema aliyoyafanya ikiwemo kushauri Watanzania kutokuwa na hulka ya kukata tamaa bali wawe na uthubutu katika kutimiza ndoto zao.
“Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako}Pumzika kwa Amani Dr. R.A Mengi,” ameandika Nape.
Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako}Pumzika kwa Amani Dr. R.A Mengi. pic.twitter.com/WJTeiLUsGY
— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) May 2, 2019
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi naye ameandika “Pumzika Kwa Amani Dr. Reginald Abraham Mengi, Mwenyekiti Mtendaji na Mmiliki wa Makampuni ya IPP Media Ni Habari mbaya kwa Taifa tunazipata ktk wakati ambao tunawahitaji watu wenye moyo km wewe. Kwa niaba ya @bavicha_taifa tunatoa pole nyingi Kwa familia na watendaji wote wa IPP.”
Absalom Kibanda, Mwenyekiti Mstaafu wa Jukwaa la Wahariri kwenye ukurasa wake wa twitter ameandika “pumzika kwa amani Regald Abraham Mengi. Ulinishika mkono kama mzazi, kiongozi, mshauri, mwalimu na rafiki wakati wa heri na nyakati za uhitaji. Umeacha alama ya pekee kwangu na kwa taifa zima.”
Pumzika kwa amani Reginald Abraham Mengi. Ulinishika mkono kama mzazi, kiongozi, mshauri, mwalimu na rafiki wakati wa heri na nyakati za uhitaji. Umeacha alama ya pekee kwangu na kwa taifa zima #RIPReginaldMengi pic.twitter.com/3OUDNC7lVe
— Absalom Kibanda (@absakibanda) May 2, 2019
Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Mwenyekiti wa BAWACHA Kitaifa kwenye ukurasa wake wa Twitter ameandika. “Nimepokea kwa masikitiko MAKUBWA SANA kifo cha ndugu Reginald Mengi. Nawapa pole sana familia, jamaa na marafiki. Mwaka 2019 unaendelea kuwa wa majonzi kwetu kama taifa, tunapoteza watu makini waliokuwa na mchango mkubwa sana katika ujenzi wa nchi yetu. Upumzike kwa Amani mkuu.”
Nimepokea kwa Masikitiko MAKUBWA SANA kifo cha Ndugu Reginald Mengi. Nawapa POLE sana FAMILIA,JAMAA na Marafiki. Mwaka 2019 unaendelea kuwa wa MAJONZI kwetu kama TAIFA,TUNAPOTEZA watu MAKINI waliokuwa na MCHANGO mkubwa SANA katika ujenzi wa NCHI yetu.Upumzike kwa AMANI Mkuu.
— Halima James Mdee (@halimamdee) May 2, 2019

Poleni sana wana familia, ndugu, jamaa, na marafiki wa @regmengi kufuatia https://t.co/K8gYzZrqvq mpendwa wetu, Reginald Mengi. Hakika, siku za maisha yetu zimehesabiwa na kuandikwa kitabuni. Ameimaliza safari yake hapa duniani. Iwe HERI kwake huko ng'ambo ya mto. RIP baba yetu. pic.twitter.com/PLzMEIonSZ
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) May 2, 2019
January Makamba, Waziri wa ofisi ya waziri mkuu mazingira na muungano ameandika katika ukurasa wake wa twitter “Pole Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins- na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi.”
Pole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins – na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi. 🙏🏾
— January Makamba (@JMakamba) May 2, 2019
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Joseph Haule mbunge wa Mikumi ameandika “R.I.P. Mzee Mengi. Umeacha Alama kubwa kwenye jamii yetu. Tangulia nasi tunafuatia.”
R.I.P Mzee Mengi..
Umeacha Alama kubwa sana kwenye jamii yetu, Tangulia Nasi tunafuatia🙏🏻🙏🏻 pic.twitter.com/kHXsXmxutT— Joseph L. Haule (@ProfessorJayTz) May 2, 2019
Leave a comment