Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Magufuli na wateule wake waonywa
Habari Mchanganyiko

Magufuli na wateule wake waonywa

Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania
Spread the love

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimesema hakitamvumilia kiongozi yoyote wa kisiasa ambaye ambaye atafanya unyanyasaji dhidi ya watumishi wa umma, anaandika Dany Tibasoni.

Chama hicho kimemtaka Rais John Magufuli kufanya kazi kwa misingi inayolinda na kuheshimu Katiba ya nchi kwa kuwa nchi inaendeshwa sheria, kanuni na taratibu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Selemani Kikingo, Mwenyekiti wa TALGWU taifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika kitaifa mjini hapa.

“Chama chetu hakina shida na utumbuaji watu wanaoitwa majipu, ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao lakini kinachotakiwa ni kuzingatia sheria na taratibu za ajira. Utumbuaji ufanyike kwa watu walio ndani ya mamlaka yake ya uteuzi lakini siyo kwa watumishi ambao wameajiriwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za ajira,” amesema.

Amedai kuwa, kwa sasa umeibuka mtindo wa baadhi ya wanasiasa kuwanyanyasa wafanyakazi ambao wameajiriwa kwa taratibu, sheria na kanuni za kazi.

“Huu mchezo wa viongozi wa kisiasa kuwanyanyasa watumishi wa serikali za mitaa unasababisha wafanyakazi kufanya kazi kwa hofu na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

“Hatutaweza kuwavumilia viongozi hao ambao wamekuwa wakiingilia sheria na taratibu za utumishi kwa kuwasimamisha kazi au kuwapa adhabu ambazo haziwahusu, ni vyema kila mmoja akaheshimu mipaka ya kila mtu katika utendaji wa kazi,” amesema Kikingo.

Kumekuwa na matukio mbalimbali ya viongozi wa kisiasa wakiwemo wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi kufanya unyanyasaji dhidi ya watumishi wa umma likiwemo tukio la mwalimu mmoja kuamuriwa kudeki darasa mbele ya wanafunzi.

Wateule hao muhimu wa Rais Magufuli pia wamekuwa wakikingiwa kifua na mamlaka yao ya uteuzi kwani hakuna hatua zozote kali za kinidhamu walizochukuliwa mpaka sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!