January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli: Mimi si mwanasiasa

Spread the love

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amesema, hajui siasa na kwamba, anachojua yeye ni kusimamia kazi za serikali. Anaadika Hamisi Mguta … (endelea).

“Mimi sio mwanasisa na sijui siasa, wala siongei siasa, hapa kazi tu,” amesema Magufuli wakati akinadi sera zake kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha leo.

Magufuli ameendelea kulalamikia Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa kushindwa kuukabili ujangili na kwamba, yeye akiingia Ikulu atahakiksha maliasili hizo zinanufaisha taifa.

Jambo lingine alilokosoa ni kukatika katika kwa umeme na kwamba, watendaji waliopo leo wakiwa kwenye serikali yake lazima wakeshe wakifanya kazi.

Hata hivyo, mgombea huyo wa urais aliingiza mdhaha pale aliposema, huwenda umeme huo kwa sasa unakatika kutokana na yeye kuanza kampeni.

“Kama matatizo ya umeme ndio haya yanayoendela basi wafanyakazi watakaokuwepo katika serikali yangu pindi wananchi watakaponipa ridhaa ya kuwa Rais, watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha umeme unapatikana,” amesema.

Hata hivyo ameonesha kukerwa na utaratibu uliopo sasa wa kutaka kuajiri wafanyakazi walio na ujuzi na kwamba, wanaotoka vyuoni watakuwa na nafasi ya kuajiriwa moja kwa moja wakati wa utawala wake, “wanafunzi wa vyuo watafanyakazi, experience (uzoefu) watapata humo humo.”

Pia kwenye mkutano huo amekosoa utaratibu unaojengwa kama mazoea kwenye Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuwaacha wawekezaji wakiajiri watu kutoka kwenye nchi zao badala ya Watanzania.

“Wawekezaji lazima waajiri Watanzania katika miradi yao ili wanufaike,” amesema.

error: Content is protected !!