February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli: Lowassa ni ‘Super Man,’ wengine wataishia magerezani

Spread the love

EDWARD Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ametajwa kuwa ni miongoni mwa wanasiasa wanaofaa kuigwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Rais John Magufuli leo Jumanne tarehe 27 Novemba mwaka huu wakati wa ufungizi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

“Maendeleo hayana chama, namwona Lowassa hapa naye yupo. Lowassa ni ‘Super Man’ ndio wanasiasa wanaofaa kuigwa. Wewe tumegombea nikakutupa nje lakini umekaa zako kimyaa. Tunahitaji wanasiasa wakomavu kama wewe,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“Muda mrefu hatujaonana kwenye shuhuli kama hizi hapa. Nakupongeza sana. Naomba mumpigie makofi. Hii ndio Tanzania mpya, vyama vyetu visiwe chanzo cha vurugu. Wengine wanasema sema lakini hawakugombea. Yeye amekaa zake kimya.”

Hata hivyo, Rais Magufuli ameeleza kukasirishwa na wanasiasa ambao hawafuati sheria za nchi na kwamba, wataishia magerezani ili wakaheshimu sheria za nchi.

Miongoni mwa wanasiasa wakubwa wa upinzani nchini waliopo mahabusu gerezani Keko ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Ester Matiko ambaye ni Mbunge wa Tarime Mjini.

error: Content is protected !!