Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Ofisi za Jiji la Dar es Salaam
Spread the love

 

JIJI la Dar es Salaam nchini Tanzania, linatarajiwa kuvunjwa ili kuokoa fedha zinazotumika kuendesha jiji hilo wakati halina miradi ya maendeleo na maeneo ya utawala. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo, imetolewa leo Jumatano tarehe 24 Februari 2021, na Rais John Magufuli wakati akizindua Daraja la Juu la Kijazi, lililopo Ubungo, jijini humo.

“Nategemea kufanya mabadiliko kidogo, mabadiliko haya ya kuwa na manispaa ambazo zinawakilisha maeneo halafu unakuwa na jiji ambalo linakaa halina maeneo yoyote, natarajia Jiji la Dar es Salaam kulivunja, nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani.”

“…lakini kuwa na madiwani wanakaa juu, wanachangiwa hela na hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu. Hili nitalikataza. Wale wanaojiandaa kuwa mameya wa Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo, wajue hilo limekwisha,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, Selemani Jafo ambaye ni Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, tayari amempa muswada wa sheria kwa ajili ya kufanya mabadiliko hayo, ambao atausaini siku yoyote kuanzia leo.
Rais Magufuli amesema, mabadiliko hayo yataruhusu manispaa moja yenye nguvu ndani ya jiji hilo kuwa jiji.

“Mjiandae kisaikolojia, wale waliokuwa wanataka Umeya wa jiji, Meya atapatikana Ilala au kutoka kwenye manispaa moja wapo hapa, na draft (muswada) nimeletewa na Jafo, nikitoka hapa nitakwenda kusaini,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, fedha zilizokuwa zikitengwa kwa ajili ya kugharamia jiji hilo, zitapelekwa katika miradi ya maendeleo.

“Ukiwa na manispaa nne au tano, halafu unakuwa na madiwani hawawakilishi maeneo yoyote. Wanawakilisha manispaa zao halafu wanatengewa bajeti, hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya barabara,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!