January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Magufuli hajatekeleza ahadi’

Spread the love

AHADI ya Rais John Magafuli kutangaza maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo, bado haijatekelezwa. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Ahadi ya Rais Magufuli ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick meck Sadick tarehe 2 Desemba mwaka huu kwenye maonesho ya 16 ya ujasiliamali ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Mnazimmoja.

Sadick aliwaahidi wajasiriamali hao kuwapatia eneo ndani ya Halmashauri ya Manispaa za Dar es Salaam ndani ya wiki mbili baada ya mkutano huo.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki na Tanzania (EACISO), Josephat Rweyemamu amesema kuwa, ahadi iliyotolewa haijatekelezwa hadi sasa na hakuna taarifa yoyote zilizotoka kwa rais wala mkuu wa mkoa.

Rweyemamu amesema kuwa wiki ijayo watafanya utaratibu wa kulifuatilia suala hilo ili kuhakikisha wanapata maeneo ya kufanyia biashara zao.

“Ushirikiano wa serikali na sekta binafsi bado ni mdogo sana hivyo kuna umuhimu wa kuwepo mamlaka ya kushughulikia sekta isiyo rasmi,” ameseama Rweyemamu.

Kuhusu ugumu wa ufanyaji kazi kwa sekta isiyo rasmi Rweyemamu amesema, bado ni changamoto kutokana na kutotengwa kwa maeneo hayo hivyo inapelekea kutembeza mikononi.

“Naiomba serikali itoe ahadi zinazotekelezeka ili kujenga imani kwa wananchi maana kauli za serikali ziwe za faraja sio usanii.” amesema Rweyemamu.

error: Content is protected !!