September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli azua tafrani Chadema

Spread the love

RAIS John Pombe Magufuli, ametoa kiasi cha Sh. 38 milioni kati ya Sh. 40 milioni, zinazotakiwa kulipia faini ya Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mamilioni hayo ya shilingi yamelipwa katika Benki ya CRDB, kupitia muamala wa mahakama ya Kisutu leo asubuhi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa.

Taarifa kutoka mmoja wa familia ya Peter Msigwa amethibitisha kuwa Rais Magufuli, amelipa kiasi hicho cha fedha, baada ya kuombwa mchango na wenzake katika familia.

“Sisi kama familia, tulikwenda kwa ndugu yetu Magufuli, tukamueleza tumekusanya Sh. 2 milioni na kwamba tunaomba naye achangie. Mheshimiwa Magufuli, akatoa mchango huo mara moja,” ameeleza ndugu mmoja wa Msigwa ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

Mbunge huyo wa Iringa Mjini, ni miongoni mwa washitakiwa Nane ambao ni viongozi wandamizi wa Chadema, waliotiwa hatiani juzi Jumanne na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washitakiwa wengine waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi 5 kia mmoja au kulipa faini ya takribani Sh. 350. milioni, ni pamoja na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho taifa.

Wengine waliohukumiwa kifungo au kulipa faini, ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; Mbunge wa Kibamba na Katibu Mkuu wa Chadema taifa, John Mnyika.

Katika orodha hiyo, wapo pia Ester Bulaya, ambaye ni mbunge wa Bunda Mjini na Vicenti Mashinji, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Dk. Mashinji alitoka gerezani jana baada ya kulipiwa faini yake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) – chama ambacho anejiunga nacho wiki mbili zilizopita. Hadi leo alasiri, wabunge waliotoka jela, ni Bulaya, Mdee na Matiko.

Mara baada ya kuzagaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, zikiwaonyesha familia ya Mchungaji Msigwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, wakithibitisha kuwa Dk. Magufuli, amemnusuru na kifungo mbunge huyo wa Chadema, mjadala mkali uliibuka huku baadhi wakimtuhumu mbunge huyo kutumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku wengine wakimtetea.

Baadhi ya waliokuwa wanamtuhumu Msigwa walifika mbali zaidi baada ya kueleza kuwa amekuwa mwepesi kutuhumu wenzake kuwa wanatumika na CCM kwa maelezo kuwa wako karibu na Rais, wakati yeye mwenyewe ni sehemu ya familia hiyo.

Msigwa na Rais Magufuli ni ndugu, wanaotokana na mmoja wa mtoto wa ndugu yake mbunge huyo kufunga ndoa na mtoto wa Magufuli.

error: Content is protected !!