Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Magufuli aweka kigingi wakwepa kodi kupitia mahakama
Habari

Magufuli aweka kigingi wakwepa kodi kupitia mahakama

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, John Magufuli ameagiza wasajili wa Mahakama ya Rufaa, kutosajili kesi za rufani zenye lengo la kuchelewesha utekelezwaji wa uamuzi wa kesi za msingi, hasa zinazohusu biashara na kodi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam..(endelea).

Agizo hilo amelitoa leo Jumatatu tarehe 1 Februari 2021, wakati akitaja changamoto za utendaji wa mhimili wa mahakama, katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

“Niwaombe wasajili ambao wako hapa mfuate sheria, hasa katika kesi ambazo haziwezi kufunguliwa rufani. Mfano kuna kesi unajua kabisa haitakiwi kufunguliwa rufani au zimezuiwa rufani, basi wasajili wasizisajili za namna hiyo.

“Kwani ni ujanja wa kuchelewesha kesi, hasa kesi zinazohusu kodi na kesi zinazohusu biashara,” ameagiza Rais Magufuli.

Hivyo, amewaagiza wasajili wa mahakama kujiridhisha na maombi wanayoletewa kwa ajili ya kufungua kesi.

“Unajua hii kesi haitakiwi ku-apeal (kukata rufaa), mhusika bado unaisajili. Ni proces (utaratibu) za kuichelewesha na watu wanakuwa wanazunguka mahakamani badala ya kwenda kushughulikia kesi,” amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hilo, Rais Magufuli ameagiza mahakama nchini kumaliza tatizo la ucheleweshaji wa uamuzi wa kesi zinazohusu biashara na mikopo.

“Changamoto nyingine ni kuhusu ucheleweshaji wa kesi, hivi punde nimetoka kuipongeza mahakama kwa kuongeza kasi, hata hivyo tatizo la ucheleweshaji bado lipo hususani kwenye mashauri yanayohusu biashara na mikopo.

“Hivyo basi, narudia kuiambia mahakama, ijipange kushughulikia changamoto hiyo niliyoeleza ambayo kwa kweli inachochea kuchelewesha ukuaji uchumi.”

Rais Magufuli amesema, tabia ya baadhi ya watu wanaodaiwa na benki kukimbilia mahakama kwa ajili ya kuchelewesha ulipaji wa madeni yao, imekuwa na athari kubwa katika uchumi wa nchi.

Ametaja athari hizo kuwa ni, kupungua kwa uwezo wa benki kutoa mikopo kwa wateja, kuongezeka gharama za riba kutokana na benki kulazimika kuongeza riba ili kufidia mikopo isiyorejeshwa.

Pia, kuongezeka kwa gharama za uendeshaji benki kutokana na taasisi hizo kuendelea kulipa riba kwa amana zilizotumika kutoa mikopo kwa wateja wenye madeni, ambao wamekimbilia mahakamani na maamuzi ya kesi zao kuchelewa kutolewa.

“Kama mnavyofahamu, serikali yetu imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi wa ksiasa na imara iliyojengwa kwa misingi ya viwanda.

“Dhamira hiyo njema haiwezi kutimia endapo hatutakuwa na taasisi imara za kifedha, hususani benki zenye ukwasi wa kutosha kwa ajili ya kutoa mikopo ya muda mrefu yenye riba nafuu,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2020, fedha kiasi cha Sh. 738.99 Bilioni ambazo zilitakiwa kulipwa katika benki nne, zinashikiliwa na watu kutokana na kesi 378 zilizofunguliwa katika mahakama mbalimbali.

Na kwamba, Benki ya Azania ina kesi 36 zilizofunguliwa na wadaiwa wake zenye thamani ya Sh. 352.27 Bilioni wakati Benki ya Maendeleo (TIB) ikiwa na kesi 44 zenye thamani ya Sh. 167.267 Bilioni. Benki ya Posta ya Tanzania (TPB) ina kesi 16 zenye thamani ya Sh. 6.2 Bil.

“Na hapa nitoe mfano wa kesi zinazofunguliwa mahakamani na wateja kwa benki ndogo tatu, TPB Azania na TIB, kwa mujibu wa taarifa za tarehe 31 Desemba 2020, Azania benki ina kesi 36 zilizofunguliwa na wadaiwa wake zenye thamani ya Sh.352.27 bilioni,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, TIB ina kesi 44 zenye thamani ya Sh.167.267 bilioni na Benki ya TPB ina kesi 16 zilizofunguliwa na wadaiwa wake zenye thamani ya Sh.6.2 bilioni na kuwa, benki hizo tatu zinadai jumla ya Sh. 525.74 Bilioni hivyo kufanya mashauri yote yaliyofunguliwa na wadaiwa kwa benki hizo kufikia Sh.525.74 Bil.

Rais Magufuli ameitaja benki ya nne iliyokwama kupata hela zake kutokana na kesi zilizofunguliwa mahakamani ni CRDB ambayo ina kesi 282, zilizofunguliwa na wadaiwa wake zenye thamani ya Sh.113.25 bilioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!