Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli awageuzia kibao wakandarasi, RC Dar ‘badilika’
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli awageuzia kibao wakandarasi, RC Dar ‘badilika’

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufulki ameagiza kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani Mbezi-Luis jijini Dar es Salaam, kukatwa fedha kama adhabu ya kuchelewa kukamilisha mradi huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Alhamisi tarehe 8 Oktoba 2020 katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho, Mbezi jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera.

Kiongozi huyo wa Tanzania amemuagiza Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Seleman Jaffo kusimamia utekelezwaji wa agizo hilo.

“Mradi huu ni mzuri lakini utekelezaji wake ni zero, haiwezekani watu watafute visingizio vya corona, Waziri huyu Contractor aanze kukatwa pesa za kuchelewa kukabidhi mradi, tukienda kwa utaratibu huu miradi mingi itahelewa,” ameagiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo Novemba 2020.

Mradi huo unaogharimu Sh.71 bilioni ulitakiwa kukamilika Julai 2020, lakini mkandarasi huyo iliomba kuukabidhi Januari 2021 kwa kisingizio cha utekelezwaji wake kusuasua kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

“Mkataba huu ulitakiwa umalizike Julai, Waziri amezungumza wanatakiwa kukabidhi Januari, hii sio haki, kuanzia Julai mpaka Januari ni miezi minne. Walitakiwa watu wawe wanaingiza pesa hapa, hiyo miezi minne nani atazilipa hizo fedha?” amehoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema “huu mradi wa Mbezi Luis Stand nitaufuatilia vizuri, halafu mtaona kama hamtazitapika kama kuna pesa zozote mlizoziweka, nimeangalia site kila mahali, Sh.71 bilion ndugu zangu ni nyingi, Sh.71 bilion?, Mimi niliidhinisha Sh.51 bilioni leo ninaambiwa Sh.71 bilion.”

Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Abubakr Kunenge kubadilika na kusimamia ipasavyo mradi huo ili ukamilike.

“Nimeambiwa hapa yatakuwa yanapark mabasi 1000, Taxi 280 kwa siku, maeneo ya bodadaboda, bajaji na maeneo ya mama lishe na baba lishe hii ni safi, ila mradi umechelewa, najua mkuu wa mkoa (Kunenge) wewe mgeni hapa lakini badilika uwe mkali usiwe Sheikh au Askofu, nataka watu wafanye kazi usiku na mchana,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema “hawa wakandarasi ni wazuri ila wamechelewesha mradi, hatuwezi kufumbia macho ujinga huu, viongozi wa Dar es Salaam mlielewe hili hizi ni fedha za Watanzania masikini, Mkurugenzi wa Jiji (Sipora) ndiye ulisaini mkataba, nataka kabla ya Novemba umalizike.”

Kiongozi huyo wan chi, amemwomba radhi Rais Chakwera kwa kuzungumza suala hilo la ucheleweshaji mbele yake akisema “naomba radhi sana Rais Chakwera, nimeumbwa kusema ukweli na nazungumza mbele ya Askofu mstaafu (Rais Chakwera). Inabidi niseme hili sivutiwi na jinsi kazi inavyoenda.”

Kwa upande wake, Rais Chakwera amesema “uzinduzi wa kituo hiki cha mabasi cha Kimataifa ni ushahidi watu wanaweza kushirikiana, Rais Magufuli kaniambia katika mabasi yanayosafiri kati ya watu 56 kwenye mabasi 15 wanakuwa Wamalawi, Wamalai wanapenda kusafiri na kuhusiana na wengine Afrika.”

“Tanzania imeonesha inaweza kuendesha miradi mkubwa kwa kutumia fedha za ndani, huu ni wakati wa Afrika kujisemea yenyewe, tuseme tunaweza kufanya ambalo Mungu ametuelekeza kufanya na pamoja tutafikia mafanikio makubwa, Hongereni sana Tanzania,” amesema Rais Chakwera.

Naye Msimamizi wa Mradi huo, Godwin Maro amesema mradi huo utakiwa na majengo ya kutoa huduma mbalimbali, ikiwemo malazi, chakula Kituo cha Polisi na huduma nyingine za kijamii.

Amesema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 108 na magari binafsi zaidi ya 200 kwa siku.

“Hili jengo litakuwa na ghorofa saba na chini ya sakafu kutakuwa na huduma mbali mbali ya maduka na katikati itakuwa sehemu ya kukaa abiria na wafanyabishara wadogo, kutakuwa na jengo la utawala lenye ghorofa tano, kituo cha polisi na vyumba vya hoteli,” amesema Maro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!