January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli atiwa ‘changa la macho’ Dodoma

Spread the love

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amedanganywa kuhusu mwenendo wa mtu aliyejitambulisha kwa viongozi wa CCM kuwa ni kiongozi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na msimamizi wa kampeni ya mgombea ubunge jimbo la Dodoma mjini. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Zoya alipopandishwa jukwaani siku Dk. Magufuli alipohutubia mkutano mkubwa wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kwamba yeye ni Katibu Mwenezi wa Chadema ngazi ya Wilaya na pia msimamizi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Dodoma mjini (Chadema), Benson Kigaila.

Mwandishi wa habari hizi kwa uchunguzi alioufanya, amethibitisha kuwa Zoya hakuwa na wadhifa huo na wala hakuwa msimamizi wa kampeni za Kigaila.

Taarifa za uongozi wa Chadema mkoani zinasema Zoya alikuwa mwanachama wa kawaida ambaye aliwahi kushika kuwa Katibu Mwenezi ngazi ya Kata ya Chang’ombe.

Imebainika kwamba Zoya alishindwa kuchukua fomu ya kugombea udiwani, badala yake akagombea udiwani katika Kata ya Majengo.

Uchunguzi umebaini zaidi kuwa Zoya amekuwa mtu maarufu wa mwenendo wa kuhamahama hata dini huku walio karibu yake wakimtaja kama mtu mpenda maslahi binafsi zaidi ya kitu kingine.

Zoya wakati akijulikana ni Mislamu, ghafla alibadilisha dini na kujiunga na Ulokole ambako pia aliacha na kurudi kuwa Muislamu; baadaye akatoka tena Uislamu na kubadilisha dini akawa Msabato anakoendelea kwa sasa.

Hatua yake ya kujitangaza kwenye mkutano wa CCM kwamba alikuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Dodoma na msimamizi wa kampeni za Kigaila, imesukuma Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA).

Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Dodoma Mjini, Fibert Musa Muhoja ambaye ni Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya Dodoma Mjini alisema Baraza la vijana Chadema(BAVICHA) Wilaya ya Dodoma mjini amesema inasikitisha unakuwa na kiongozi anayepotosha umma.

Muhoja amesema viongozi wa CCM walipo mjini Dodoma wanajua vizuri ukweli huo wa mwenendo wa Zoya lakini hawakumjulisha Magufuli, jambo ambalo Muhoja anasema viongozi hao walilifanya kwa nia ya kumzuga mgombea wao kwa maslahi binafsi ya kuonekana wamemfanyia kampeni ya Magufuli.

“Ukweli mmoja haufutiki kuhusu mwenendo wa Zoya… ni mtu anayehamahama hata dini inayohusu uhusiano wa binadamu na Mwenyezi Mungu. Mtu akiwa si muaminifu kwa Mwenyezi Mungu hashangazi kuwa mbabaishaji kwa binadamu wenzake,” alisema.

“Huyu Zoya tunamjua na hata viongozi wa CCM hapa Dodoma wanamjua vizuri, ni mkazi wa Chang’o mbe na kazi yake ni fundi cherehani na elimu yake ni darasa la saba,” amesema.

“Mwaka 2010 Khalid Zoya alinunuliwa na kupoteza Kata ya Majengo kwa mgombea wa CCM ambaye kwa sasa anatetea nafasi hiyo Msinta Mayauyau.

 

“Katibu Mkuu wa CCM aliyekuwepo kabla ya Wilson Mukama, Luteni Yusuph Makamba alimpatia Zoya vyerehani viwili na shilingi laki tatu ambayo pia walidhulumiana na baada ya muda, Zoya alirudi Chadema,” alieleza Muhoja.

“Pia sisi Baraza la Vijana tumesikitishwa na yeye kujipa vyeo ambavyo kimsingi hajapata kushika akiwa Chadema. Mpaka sasa tunavyoongea katibu mwenezi wa Wilaya ya Dodoma Mjini ni Juma Bika Mtaalam, japo alisimamishwa uongozi kwa muda na ndio amekuwa Kampeni Meneja wa mgombea ubunge jimbo la Bahi, Mathias Lyamunda,” amesema.

“Suala la yeye kujiita kampeni Meneja wa mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma Mjini ni la uongo na tunaomba wananchi wampuuze maana ni cheo alichokuwa akikitaka na sisi tunaamua kwa vikao, hakuna muhtasari wa kikao chochote uliopitisha jina lake kuwa Kampeni Meneja…

“Tunajua amepewa shilingi laki 7 na kuahidiwa kununuliwa vyerahani vingine viwili, na kupangishiwa fremu ya ofisi ya kushonea,” amesema Muhoja.

Zoya pia aligombea ukatibu wa Bahi mwaka 2010 akashindwa, aligombea mara mbili udiwani Kata ya Chang’ombe bila ya mafanikio na alipotaka kugombea Kata ya Majengo akashindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama.

“Kama alipitishwa kuwa mgombea angethubutu kuonesha ushahidi wake wa maandishi,” amesema Muhoja na kusikitika kuwa siasa za kilaghai hazina maana yoyote.

Kigaila naye amemkana Zoya kwamba si kampeni meneja wake na hakuna kikao cha ngazi yoyote Chadema kilichompitisha.

Kuhusu tuhuma za kutishiwa kwa Zoya, Kigaila alisema hakuna mtu anayeweza kumtishia Zoya kwa sababu chama ni taasisi na si mtu.

error: Content is protected !!