August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli atisha wafanyabiashara wa sukari

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, wafanyabishara wanaochezea serikali yake kwa kuficha sukari, akiwabaini hawatafanya bishara tena tena nchini, anaandika Wolfram Mwalongo.

Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Hanang, Katesh mkoani Manyara leo wakati akielekea Arusha, amewataka wafanyabiashara kutoa sukari ilifichwa kwenye maghala na iuzwe kwa wananchi kwa bei iliyapangwa.

Rais Magufuli amesema, wafanyabiashara wanaoficha sukari ni wahujumu uchumi hivyo ameagiza vyombo vya dola viwafuatilie wote walio ficha sukari.

Aidha amewahakikishia wananchi kuwa, serikali yake haishindwi kuagiza sukari nje na kwamba, amemwagiza Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ili kuhakikisha inaletwa sukari ya kutosha na wananchi watapata kwa bei ya chini.

error: Content is protected !!