August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli ateua mshauri wake na naibu mwanasheria mkuu

Spread the love

RAIS John Magufuli amemteua amemteua Gerson Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuziba nafasi iliyoachwa na Dkt. Tulia Akson ambaye kwa sasa ni Naibu Spika wa Bunge. Anaandika Pendo Omary.

Katika taarifa iliyotolewa na leo kwa vyombo vya habari na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu inasema “kabla ya uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (cabinet Clerk).”
Aidha, taarifa hiyo inasema Rais Magufuli pia “amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa mshauri wa Rais masuala ya uchumi. Kabla ya uteuzi huo Profesa Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.”
error: Content is protected !!