August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli ashiriki kumbukumbu ya mauaji ya kimbari

Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ameshiriki uzinduzi wa kumbukumbu za mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 1,000,000 waliuawa.

Ziara ya Mgufuli nchini Rwanda ni ya kwanza tangu kuapishwa Novemba 5 mwaka2015 kwa madai kuwa ameazimia kubana matumizi kwa kufuta safari za nje zisizo na tija kwa viongozi wote wa serikali.

Magufuli yupo nchini humo kwa ziara ya siku mbili akiwa ameambatana na Mkewe mama Janeth, pamoja na Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa

error: Content is protected !!