Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli apeleka neema Ukerewe
Habari za Siasa

Magufuli apeleka neema Ukerewe

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amepandisha hadhi kituo cha afya cha Bwisya kilichoko Ukara wilayani Ukerewe jijini Mwanza kiwe na hadhi ya hospitali ya wilaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ukerewe … (endelea).

Hayo yamesemwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Bwisya kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya bandarini jana mchana Jumatano, tarehe 23 Septemba 2020.

Alisema awali kituo hicho cha afya zamani kilikuwa zahanati lakini ikapandishwa hadhi ili kuwasaidia wakazi wa tarafa ya Ukara.

“Tunataka wananchi wasihangaike kwenda hadi Nansio yalipo makao makuu ya wilaya hii. Huduma zitatolewa hapahapa. Hiyo maana yake, majengo ya tiba yataongezwa na vitengo vya huduma vitaongezwa na madaktari bingwa wataletwa wakae hapa.”

Majaliwa alisema, ili kufanikisha hilo kwa haraka hospitali ya wilaya ya Ukerewe ambayo iko Nansio nayo pia itapandishwa na kuwa na hadhi ya Hospitali ya Mkoa.

Kupandishwa hadhi kwa kituo hicho cha afya, kutawasadia wakazi wa Ukara ambao walikuwa wanapaswa kufuata huduma za rufaa Nansio ambako ni umbali wa kilomita 30 au Mwanza mjini ambako ni umbali wa kilomita 75.9.

“Hapa Bwisya zililetwa Sh.1.4 bilioni za kupandisha hadhi kutoka zahanati na kufikia kuwa kituo cha afya. Hospitali nyingi za wilaya hapa nchini zimepatiwa Sh.1.8 bilioni, kwa hiyo na ninyi hapa mtapatiwa fedha ili majengo yanayohitajika yaweze kukamilika,” alisema.

Majaliwa ambaye yuko mkoani Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea ubunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi na diwani wa Bwisya, Dickson Sute. Madiwani wengine watatu wa tarafa ya Ukara, wamepita bila kupingwa.

Akitoa ufafanuzi kwenye sekta hiyo ya afya, Majaliwa alisema Sh.2.95 bilioni zimetolewa wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya ujenzi wa majengo tano ambayo ni maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mganga katika vituo vya afya vya Bwisya, Kagunguli na Muriti.

“Kituo cha Afya cha Bwisya kilipatiwa Sh.1.4 bilioni ambapo ujenzi na upanuzi umekamilika. Kituo cha Afya Kagunguli kilipatiwa Sh.322 milioni ambapo ujenzi chumba cha kisasa cha upasuaji umekamilika na Kituo cha Afya Muriti kilipatiwa Sh.967 milioni ambapo ujenzi majengo ya RCH, upasuaji na wodi ya wazazi yote yamekamilika,” amesema.

Kuhusu ununuzi wa dawa na vifaa tiba, Majaliwa alisema Sh.3.9 bilioni zimetolewa kwa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kwa kipindi cha 2015/2016 – 2019/2020 ambapo wastani wa bajeti ya dawa kwa mwezi ulikuwa ni Sh.63 milioni.

 

Akizungumzia usafiri wa majini katika maziwa mito na bahari kama ilivyoainishwa kwenue Ilani ya Uchaguzi uk. 69 -70, Majaliwa alisema ujenzi wa vivuko vinne ambavyo vitatoa huduma katika maeneo ya Bugolora – Ukara (Mwanza), Kayenze – Bezi (Mwanza), Nyamisati – Mafia (Pwani) na Nkome – Chato -Buharamba (Geita) unaoendelea.

Alisema Serikali imekamilisha ununuzi wa boti tatu za uokozi kwa ajili ya maeneo ya Ilugwa – Ukara (Ukerewe), Nafuba na Gana katika kisiwa cha Ukerewe.

“Ili kuimarisha usafiri katika maziwa na mito, Serikali imeanza ujenzi wa vivuko na maegesho muhimu nchini ikiwemo Ujenzi wa maegesho ya Ilugwa (Ukerewe) pamoja na vivuko vya Bwiro–Bukondo (Ukerewe), Irugwa–Murutanga (Ukererwe) na Kakuro–Gana (Ukerewe). Na hii iko kwenye ukurasa wa 83 wa Ilani yetu,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!