Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli amwapisha mrithi aliyeshindwa kuapa
Habari za Siasa

Magufuli amwapisha mrithi aliyeshindwa kuapa

Rais John Magufuli
Spread the love

PROFESA Shukrani Manya, leo Ijumaa tarehe 11 Desemba 2020, inaweza kuwa siku ya historia katika maisha yake, baada ya kula viapo viwili tofauti ndani ya siku moja. Anaripoti Brightnes Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Profesa Manya aliyezaliwa tarehe 5 Machi 1973 Ukerewe jijini Mwanza, ndani ya siku moja, ameapishwa na Spika Job Ndugai kuwa Mbunge wa Tanzania kisha, akaapishwa kuwa naibu waziri wa madini.

Ni ndani ya siku moja ya leo Ijumaa, Rais Magufuli amemteua Profesa Manya kuwa mbunge wa kuteuliwa, kisha akamteua kuwa naibu waziri wa madini, akichukua nafasi ya Francis Ndulane, aliyeshindwa kuapa vizuri kiapo cha naibu waziri.

Ndulane ambaye ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoa wa Lindi, alikutwa na kadhia hiyo, Jumatano ya tarehe 9 Desemba 2020, wakati Rais Magufuli akiwaapisha mawaziri 21 na naibu mawaziri 22 Ikulu ya Chamwino, Dodoma,

Baada ya kuambiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kurejea upya kuapa, alionekana kuweweseka ndipo, Balozi Kijazi alimweleza akapumzike kwanza huku Rais Magufuli akiahidi kuteua mtu mwingine “anayejua kuapa vizuri.”

Rais Magufuli alisema, atafanya uteuzi wa naibu waziri mwingine wa madini ambaye ataweza kusoma vizuri nyaraka na Ndulane atasalia na nafasi yake ya ubunge.

https://youtu.be/DkyGnyw5Cdg

Awali, mida ya saa tano asubuhi, Spika Job Ndugai alimwapisha Profesa Manya kuwa Mbunge wa Bunge la Tanzania, hafla iliyofanyika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Profesa Manya  aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania alimshukuru Mungu “kwani yeye ndiye hupanga majira na nyakati za mwanadamu.”

“Nimeshukuru Rais Magufuli kwa kuniteua kuwa mbunge na nitafanya majukumu yangu ya ubunge kwa uadilifu ili kwa pamoja tulisukume gurudumu mbele la Taifa letu,” alisema Profesa Manya, aliyekuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Mara baada ya kuapishwa na Rais Magufuli, Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema, Profesa Manya ni mzoefu katika sekta ya madini, “tunampongeza kwa kuteuliwa kuwa mbunge na naibu waziri.”

Biteko amesema, Profesa Manya anapaswa kutambua kwamba, anahudumu nafasi ndani ya sekta ya madini “ambayo wewe Rais unaijua, sisi tutakwenda kufanya kazi” kadri tunavyoweza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!