May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amteua Dk. Bashiru kumrithi Balozi Kijazi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dk. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaan … (endelea). 

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Bashiru alikuwa Katibu Mkuu wa chama tawala- Chama Chama Mapinduzi (CCM).

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, leo Ijumaa usiku tarehe 26 Februari 2021, imesema, Dk. Bashiru, anachukua nafasi iliyoachwa na Balozi John Kijazi, aliyefariki dunia.

Balozi Kijazi, alifariki dunia tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dodoma na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao, Korogwe mkoani Tanga.

Wakati huo huo, Msigwa amesema, Rais Magufuli amemteua Dk. Bashiru kuwa Balozi.

Uteuzi wa Dk. Bashiru unaanza leo na ataapishwa kesho Jumamosi saa 3:00 asubuhi Ikulu, jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!